October 04, 2021

YANGA NA MZIKI WA MSIMU AMA NYUZI ZITAKATIKA?


Na John Richard Marwa


Mziki umelia nyuzi zimeimba jangwani ni kinanda. Soka la kukaanga chipsi majukwani limepata wenyewe.

Khalid Aucho, Yanick Bangala, Diarra na Feisal Salum wamekoleza sana one two wanacheza kwanza akilini kisha wanacheza kwa miguu yao hapa ndio yanga Ina mabadiliko ya yaliyopita na yajayo.

Aucho anafanya kila kitu rahisi ndani ya Uwanja, yaani hata kama huna control nzuri basi pasi yake inakufundisha ku control mpira ndani ya mchezo.

Football is the game of calculation, Mtrix equation na probability action katika hivyo vitu vitatu yanga wanazidi kuimarika.

Ukiacha calculation za muda kwenye akili na muda kwenye matendo basi muda kwenye matendo ndio silaha tosha yaani probability action.

Probability action ni kuwnaia kila tukio lililoko mbele yako katika kila sekunde kihisia na kimatendo.

Eneo la mbele bado Kocha Nabi anahitaji kufanya kazi nzuri jinsi gani washambuliajj wanasoma mikimbio na kuwa na probability action katika kuwnia nafasi sahihi.

Katika Dakika 45 hadi 60 Yanga wanakuwa na kiwango Bora sana ila baada ya hapo wachezaji wanakata upepo.

Hii sio ishara nzuri kwa timu inayohitaji ubingwa, inayohitaji kujipambanua kuwa klabu kubwa lazima iwe bora muda wote wa mchezo.

Mpaka sasa kuna Yanga mbili katika kila mchezo walioucheza Yanga ya kipindi cha kwanza na Yanga ya kipindi cha pili ni Yanga zenye vinasaba tofauti.

Ni jukumua la benchi la ufundi kuhakikisha wachezaji wanakuwa na uwezo wa kuzikabili Dakika 90 katika ubora ule ule, vinginevyo Vilio na masimango yataendelea bila kukoma na ubingwa watausikia kwenye Bomba.

No comments:

Post a Comment

Pages