NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
VIJANA nchini wameshauriwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika sekta ya michezo hasa katika mpira wa miguu.
Rai hiyo ameitoa Mbunge wa Jimbo la Welezo Mhe.Maulid Saleh Ali wakati akikagua matengenezo ya uwanja wa mpira wa Matemwe ulipo katika Jimbo hilo.
Amesema kuwa michezo kwa sasa ni miongoni mwa sekta inayotoa ajira nyingi kwa vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali kujipatia fedha.
Aliwambia vijana hao waendelee kutumia vizuri uwanja huo kwa kufanya mazoezi na kushindana na timu mbalimbali za majimbo jirani ili wapatikane wachezaji wenye vipaji na uwezo mzuri wa kucheza mpira.
Amewaahidi vijana hao kuwa ataendelea kuwaunga mkono katika masuala mbalimbali yakiwemo ya michezo ili kwenda sambamba na matakwa ya Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Alieleza
kwamba ametoa vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na kudhamini ligi za jimbo
hilo za vijana pamoja na kuibua vipaji vya vijana wadogo ambao kwa sasa wana
uwezo mzuri wa kucheza mpira na michezo mingine.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa Jimbo hilo Ayoub Saleh Ayoub, alisema uwanja huo ulikuwa na umeanza kuharibiwa na maji ya mvua hivyo wanaufanyia matengenezo ili vijana wapate uwanja wenye viwango.
Aidha alisema mbunge huyo amekuwa akijitolea kufanikisha masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo hivyo amewasihi viongozi wengine kuiga mfano huo wa kiutendaji.
Kwa upande wake Farid Juma Issa ambaye ni miongoni mwa vijana wanaotumia uwanja huo, alimpongeza mbunge huyo kwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kutengeneza uwanja huo.
Picha no.02- MBUNGE wa Jimbo la Welezo Mhe. Maulid Saleh Ali,akishirikiana na wananchi na mafundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar(ZAWA) kubeba mabomba ya kusambaza maji kwa ajili ya kuungwa.
No comments:
Post a Comment