January 08, 2022

Halmashauri ya Chamwino yapewa bl. 2.92 ujenzi wa madarasa


Mkuu Mkoa wa Dodoma Anthony Mataka (kushoto) akizindua moja ya vyumba vya madarasa wilayani Chamwino (kulia) ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Dodoma Godwin  ),Godwin Mkanwa.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

SERIKALI imetoa shilingi bilioni 2.92 za mradi wa UVIKO-19  kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 146 katika Halamashauri ya Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

Pia wananchi  wa Halamashauri ya hiyo  wametakiwa kuwahamashisha watoto wao kusoma katika madarasa hayo yaliyojengwa kwa mradi wa UVIKO-19 ili yalete tija na kwamba kama hawatasoma Madarasa hayao hayatakuwa na maana.

Akizungumza jana jijini Dodoma katika  ziara ya Mkuu Mkoa wa Dodoma Anthony Mataka wakati akizindua vyumba vya madarasa wilayani humo Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amesema moja ya Halmashauri iliyopata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ni Wilaya ya Chamwino.

Msuya amesema kuwa Wilaya hiyo imewekewa bajeti kubwa katika mradi wa ujuenzi wa madarasa ambayo inatokana na fedha za UVIKO-19.

"Nampongeza Rais wetu Samia Suluhu Hasaan pamoja na serikali yake kwa ujenzi huu wa madarasa pia naishukuru kwa kutupatia Halmashauri yetu shilingi bilioni 2.92 hili ni jambo la kujivunia," amesema Mkuu wa Wilaya hiyo.

Aidha amewapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuwa walinzi wa vifaa vya ujenzi pamoja na miundombinu.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari ya Msanga Hatibu Luwumba amesema shule hiyo imepewa kiasi cha shilingi milioni 60 na kwamba wananchi walichangia milioni 1.6.

Pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma (CCM),Godwin Mkanwa amesema mafundi wanaojenga madarasa kupitia mradi wa UVIKO-19 wamejengewa uwezo na serikali.

Amesema katika ujenzi wa madarasa wa kata ya Msanga  nidhamu ya matumizi ya fedha hizo yamekuwa ni ya nidhamu kubwa.

"Nawapongeza wananchi na viongozi wa Wilaya hii katika kujitolea kuchangia ujenzi wa madarasa," amesema.

Awali akizindua madasara hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mataka ameipongeza serikali kwa mradi huo na kwamba wananchi wahakikishe hakuna mtoto anaebaki nyumbani bila kusoma.

No comments:

Post a Comment

Pages