Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mwili wa Baba wa Balozi Dk. John Nchimbi ulizikwa jana, katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali wakiwemo Mawaziri na Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson.
Mazishi hayo ambayo tunaweza kusema kuwa yalitikisha Jiji la Dar es Salaam, yalifanywa kwa heshima zote za Jeshi la Polisi, kwa kuwa Mzee Nchimbi ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77, mbali na kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya CCM ikiwemo Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Katibu wa CCM wa mikoa ya Kigoma, Singida na Dar es Salaam na kuwa mkufunzi wa vyuo vya Chama vya Ilonga na Kivukoni alikuwa ni Kamanda wa Polisi mstaafu ambaye alihudumu katika mikoa ya Morogoro na Mtwara.
Mfululizo wa hatua mbalimbali za mazishi hayo ulianzia nyumbani k wake Marehemu, Tabata Kisiwani ambako waombolezaji walikusanyika kwa maelfu kabla ya kwenda katika Kanisa Katoliki la Apio, katika eneo hilo la Tabata ambako Ilifanyika Misa ya wafu na baadaye Viongozi, Ndugu Jamaa na marafiki wa familia wakapewa nafasi ya kutoa heshima za mwisho.
Katika utoaji wa heshima za mwwisho Kanisani hapo, Ndugu wa karibu hawakutoa heshima hizo kwa mwili wa marehemu kwa kuwa mapema mwili ukiwa nyumbani walipata fursa ya kutoa heshima za mwisho.
Baada ya kutoka Kanisani mwili ulipelekwa Makaburi ya Kinondoni, kwa ajili ya maziko, ambako wakati wa maziko Polisi walifanya paredi maalum ambalo liliambatana na kupigwa mabomu kumi (10) kwa heshima ya Marehemu Mzee Nchini ambaye katika kuhudumu katika Jeshi la Polisi alistaafu akiwa na cheo cha Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo.
Zifuatazo ni picha zaidi ya 300, za matukio mbali mbali yaliyojiri wakati wa mazishi hao, Tafadhai tazama moja baada ya nyingine hapo👇
Dk. Mndolwa akisindikizwa kuingia msibani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Edmund Mndolwa, akisaini Kitabu cha maomolezo.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Edmund Mndolwa akisalimiana na muomboezaji mwenzake William Ngeleja.Kada wa CCM Shy Rose Bhanji akisaini kitabu cha maombolezo.
Jirani wa nyumbani kwa marehemu Mzee Nchimbi Max Komba akibadilishana mawazo na waombolezaji wenzake.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akikaribishwa na Mbunge mstaafu wa Mbinga Sixtus Mapunda na Vijana wa CCM alipowasilimsibani nyumbani kwa marehemu John Alphonso Nchini, Tabata Kisiwani jijini Dar es Salaam, kushiriki mazishi, janaWaziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, akisaini kitabu cha maombolezo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, akimsikiliza kwa makini Mbunge mstaafu wa Mbinga Sixtus mapunda alipowasili msimbani.Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akisalimiana na waombolezaji wenzake.Mbunge wa Sengerema William Ngelea akimpa pole Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi. Katikati ni Sixtus Mapunda.
Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na muomblezaji Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa. Kushoto ni Waziri Nape Nnauye akimsubiri kwa hamu Balozi Dk. Nchini ili ampe pole.
Waziri Nape alipofikiwa akamkumbatia Balozi Dk. Nchini kumsalimia na kumpa pole.
"Pole Sana kaka", Nape akasema
Kisha akamnong'oneza jambo huku wakifurahi kidogo kupunguza machungu ya msiba.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akimsalimia waziri Nape.
Waziri Nape na Waziri Bashe wakimpa pole kwa pamoja Balozi Dk. Nchimbi.
Waziri Nape na Waziri Bashe wakizungumza.
Waombolezaji kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wakimpa pole Balozi Dk. Nchini. Nchimbi amewahi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM.
Muombolezaji akimpa pole Balozi Dk. Nchimbi
Wajukuu wa Marehemu Mzee Nchimbi wakiwa msibani.
Waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu.
Waombolezaji
Waombolezaji.
Waombolezaji.
Waombolezaji Vicky Kamata, Syrose Bhanji na Dada Ashura wakiwa msibani
Wanafamilia ya Marehemu Mzee John Nchimbi wakiwa msibani.
No comments:
Post a Comment