January 09, 2022

RUWASA ya saini mikataba yenye thamani zaidi ya bl. 3.6

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mataka wa tatu (kulia), kwa  waliosimama akishuhudia utiaji saini wa miradi ya ujenzi wa maji mkoani humo yenye thamani zaidi ya bilioni 3.6.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

JUMLA ya mikataba 4  ya ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani zaidi  ya bilioni 3.6 imesainiwa jijini Dodoma ambayo imegawanyika katika makundi mawili.

Makundi hayo ni bajeti ya kawaida mikataba miwili yenye thamani ya bilioni 2.7  na mradi wa UVIKO-19 mikataba miwili yenye thamani ya bilioni 1.9.

Akizungumza jijini Dodoma jana  katika hafla fupi ya kusaini mikataba hiyo Meneja wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma (RUWASA), Dk.Godfrey Mbabaye amesema miradi ya UVIKO-19 Mkoa huo umetengewa zaidi ya bilioni  3.9 kutekeleza miradi 8 katika Wilaya  5.

Meneja huyo amezitaja Wilaya hizo kuwa ni Kongwa, Mpwapwa, Chemba, Kondoa na  Chamwino ambayo imesainiwa na kwamba  mikataba  miwili ya Wilaya za Chamwino, Chemba na Kondoa yenye jumla ya miradi mitano.

" Thamani ya miradi hii ni bilioni 1.9 na mkataba mmoja wenye miradi mitatu ya Wilaya za Kongwa na Chamwino wenye thamani ya bilioni 1.6 umepelekwa kwa mwanasheria  Mkuu wa Serikali  kwa ajili ya kufanyiwa upekuzi na unategemewa kusainiwa kabla ya Januari 16 mwaka huu, " amesema Dk.Mbabaye.

Ameongeza kuwa miradi inayotumia fedha za ndani imesainiwa miwili ambayo itatekelezwa katika Wilaya za Chamwino na Kondoa ina jumla ya thamani zaidi bilioni  1. 7.

Dk.Mbabaye amefafanua kuwa hiyo ni sehemu ya mikataba 34 ya maji ambayo inategemewa katika Mkoa wa Dodoma.

"Kati ya zabuni 34 zilizotangazwa 18 zilitangazwa zipo katika hatua mbalimbali za kukamilisha taratibu za utiaji saini. Zabuni 7 zinategemewa kutiwa saini Januari 16, mwaka huu  na 11 zinategemewa kutiwa saini February 25 mwaka huu, amesema.

Amesema miradi 12 ambayo haijatangazwa imepewa kibali cha kuendelea na taratibu za manunuzi na kwamba miradi hiyo katika bajeti ya mwaka huu ikikamilika itaweza kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka asilimia 64.6 ya sasa  hadi 66 ifikapo Juni.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mataka amesema kuwa Wakandarasi hao kama hawajamaliza miradi hiyo ndani ya muda hawataweza tena kupatiwa zabuni nyingine.

" Lazima tuwe na utamaduni wa kwenda na muda  ili kukamilisha miradi kwa wakati leo tumekutana kwa ajili ya miradi hii," amesema Mataka.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatma Maganga amesema wameshuhudia uwekaji saini wa mikataba mikubwa ya maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3.6.

"Hi ni fedha ndefu ni fedha kubwa hivyo tunaamini fedha hii itaenda kuleta faida. Tuna kwenda kutekeleza miradi hii  kwa uzalendo mkubwa tunachotaka Dodoma ni miradi hii ikamilike kwa wakati," amesema Katibu Tawala huyo.

Ameongeza kuwa wakati wa longo longo umekwisha ni wakati wa kuonesha matokea, akina mama wanahangaika maji  na kwamba serikali imefanya kazi yake ya kutoa fedha.

Katibu Tawala huyo amesema wao kama  viongozi watasimamia wakandarasi  na wanategemea ndani ya muda uliowekwa itakamilika.

Aidha ameishukuru serikali na msimamizi wake Rais Samia Suluhu Hasaan kwa kuiona tena  Dodoma katika nyanja ya maji.

No comments:

Post a Comment

Pages