Na Dotto Mwaibale, Singida.
SENETI ya Vyuo na Vyuo Vikuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imetoa pongezi za dhatia Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini wa Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Tanzania kwa kumpitisha Dk.Tulia Ackson kuwa mgombea wa nafasi ya Uspika kwa tiketi ya chama hicho.
Akizungumza kwa niaba ya UVCCM Katibu wa Seneti Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Singida, Paulo Dotto alimpongeza kamati hiyo kwa kumpitisha Tulia kugombea nafasi hiyo.
"Tunatambua kamati kuu ilikuwa na kazi kubwa na nzito ya kuhakikisha inampata mgombea bora kati ya 71 waliojitokeza tuna amini Wana CCM wote walikuwa bora na wazuri na kwamba mchakato umeonesha dhahiri CCM imekomaa kidemokrasia na inapendwa na kukubalika hasa ikizingatiwa idadi ya waliochukua fomu kuwa kubwa kuliko marajio yetu" alisema Dotto.
Alisema CCM imefanikiwa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kwa uwazi na kufuata sheria, kanuni na taratibu zote baada ya aliyekuwa kuwa akihudumu nafasi hiyo Job Ndugai kujiuzulu ambapo kamati hiyo ilimpitisha Dk.Tulia Ackson kwa kauli moja tofauti na vyama vingine ambavyo taratibu zao hazipo wazi.
Aidha Dotto alisema CCM inaamini kuwa kila mtu ana nafasi ya sawa ya kuchaguliwa na kuwa kiongozi bila kujali jinsia, kabila, ukanda na matabaka.
" Ikumbukwe Spika mstaafu Anne Makinda aliteuliwa na Kamati Kuu na baadae kuungwa mkono na wabunge wote wakiwemo wa upinzani na alitekeleza ipasavyo majukumu yake tofauti na matarajio ya wengi hivyo kwa uamuzi wa kumteua Dk. Tulia ni sahihi na ni imani yetu amekuwa na sifa za ziada kuliko wengine.
Baadhi ya sifa hizo ni wakati wa Bunge Maalumu la Katiba alikuwa mbele katika suala zima la kulinda maslahi ya nchi, amemudu kuitendea haki nafasi yake ya Unaibu Spika katika kipindi kigumu cha Serikali ya awamu ya Tano kilichokuwa na upinzani mkali huku akishiriana kwa karibu na Spika mstaafu Job Ndugai.
Katibu wa Hamasa na Chipukizi (CCM) Manispaa ya Singida Yahaya Njiku alisema Vijana wa Manispaa hiyo wataendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
No comments:
Post a Comment