January 17, 2022

Serikali kupunguza gharama za matibabu na vifo kwa Watanzania


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa  viongozi wa idara ya kinga na kufanya mapitio ya pamoja kuhusu mafanikio, changamoto na vipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga nchini.

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu leo amekutana na Viongozi wa Idara ya kinga na  kufanya mapitio ya pamoja kuhusu mafanikio ,changamoto na vipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga nchini ili kupunguza maradhi,ulemavu.

Pamoja  na kupunguza gharama za matibabu na vifo miongoni mwa watanzania.

Kikao hicho kimefanyika mapema Leo mapema Januari 17, 2022, katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifello Sichalwe.

Katika kikao hicho,Ummy amesisitiza juu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi ili kupunguza kero na malalamiko katika jamii katika nyanja zote, ikiwemo katika huduma za mama na mtoto na huduma za lishe.

Mapitio yaliyofanywa kwenye kikao ni pamoja na ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ,huduma za chanjo,afya ya uzazi na mtoto,huduma za lishe,afya mazingira,Elimu ya Afya kwa Umma.

Aidha, wamejadili mikakati mbalimbali ya mapambano dhidi ya UVIKO-19, Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(NTDs), Malaria,Kifua Kikuu na Ukoma na UKIMWI.

No comments:

Post a Comment

Pages