HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 10, 2022

Mhandisi Mtambo: Wanawake ni mtaji wa kisiasa


Mhandisi Mohamed Mtambo akizungumzia siku ya wanawake Duniani Machi 8, 2022 Wilayani Mkuranga Mkoa wa  Pwani.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo wakiwa na zawadi za kuwapatia wanawake waliojifungua katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8 mwaka huu.


Na Arodia Peter, MKURANGA 


Katibu wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mhandisi Mohamed Mtambo amesema wanawake ni kundi la kipekee katika kufikia malengo ya kitaasisi zikiwamo za kisiasa.


Amesema wanawake wakiwezeshwa na kuandaliwa vizuri kielimu na kiuchumi hakuna kitu kinaweza kuwashinda.


Mhandisi Mtambo aliyasema hayo katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi  8,2022 wilayani Mkuranga mkoani Pwani.


Akiwa mgeni mwalikwa alisema yeye kama mwanasiasa anatambua na ku heshimu jitihada kubwa zinazofanywa na wanawake mkoani humo licha ya kuwapo changamoto mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.


Alisema usawa wa kijinsia ni nyenzo muhimu endapo itatumika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.


"Binafsi nashukuru chama changu cha ACT Wazalendo Ngome ya Wanawake Taifa kwa kukubali kusherehekea nasi Siku hii muhimu naya kipekee kwa mama zetu, dada zetu wa mkoa wetu wa Pwani.


"Hatua hii inatupa nguvu watu wa Pwani kwani itaongeza chachu ya mapambano ya haki na usawa kwenye eneo hili.


"Wote tunatambua kwamba mazingira tuliyo nayo sasa niya dunia jumuishi..hivyo  bila hawa wanawake hata mafanikio ya kisiasa hayawezi kupatikana " alisema Mtambo.


Aidha Mtambo ambaye amepata kugombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga (ACT) mwaka 2020, alisema jimbo hilo linakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji, upungufu wa hospitali, vituo vya  afya pamoja na taasisi za mikopo ili kuwezesha wananchi kiuchumi.


Mgeni rasmi katika Kongamano hilo kubwa alikuwa Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo (Bara), Dorothy Semu pamoja na viongozi wa Ngome ya Wanawake Taifa. 

No comments:

Post a Comment

Pages