April 28, 2022

GF TRUCKS - YAFUTURISHA WADAU NA WAFANYAKAZI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Gf Truks & Equipments Ltd, Mehboob Karmali akimkaribisha Shekh wa mskiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Marekani Shekh, Syed Ali Raza Rizvi wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar Salaam.

Shekh wa mskiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Marekani Shekh, Syed Ali Raza Rizvi akiangalia zawadi ya Tasbihi  bada ya kupewa  na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Gf Truks & Equipments Ltd, Mehboob Karmali wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar Salaam.

Mkurugenzi wa kampuni ya Gf Truks & Equipment’s Ltd, Imran Karmali  akimwangalia mfanyaklazi wa kampuni, Isack Shehemba hiyo aliyejishindia Redio (saboufa) wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar Salaam.

Baadhi ya wadau na wafanyakazi wakichukua chakula.
 

Dar es Salaam, Tanzania

Waislamu na wanajamii kwa ujumla wametakiwa kuutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kubadili tabia kwa kutenda yaliyo mema na kuyaendeleza hata baada ya kumalizika mfungo.

Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni GF Truck & Equipments LTD, Mehboob Karmali mara baada ya kufuturisha wadau mbali mbali na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Alisema mara nyingi mwezi huo umekuwa ukileta utulivu katika jamii, “Haijalishi ni kijana, mzee, Muislamu na asiyekuwa mwislamu, ilimradi wengi hutulia na kuuheshimu, hivyo ni vema kuendeleza yale mema hata katika nyakati nyingine ili jamii iwe salama.

“Kipindi hiki pia ni vema kuwapa wahitaji sadaka kwa kile kidogo tutakachojaaliwa kwa sababu tunazo.

No comments:

Post a Comment

Pages