April 12, 2022

Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB waendelea kugusa wengi

Mwakilishi wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkundutsi wilayani Kasulu, Kigoma akizungumza kwa niaba ya wanafunzi walipotembelewa na maafisa wa Benki ya NMB.

Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisuke wilayani Ushetu akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo walipotembelewa na maafisa kutoka Benki ya NMB

Afisa wa Benki ya NMB kutoka idara ya uwajibikaji kwa jamii, Aloyce Kikois akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Ushokola walipotemebelea shule hiyo.

 

Kupitia sera yake ya uwajibikaji kwa jamii (CSR), Benki ya NMB imetenga asilimia moja ya faida baada ya kodi kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali hususani katika sekta za elimu, afya na majanga.

Katika ziara ya watumishi wa Benki hiyo kwa mikoa wa Tabora, Kigoma na Shinyanga, wameshuhudia wakazi wakinufaika na misaada hiyo na kueleza namna ambavyo mchango wa NMB umekuwa chachu ya hatua kubwa za kimaendeleo kwao na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wa elimu, mashuhuda wameelezea kuwa, tangu NMB iwape viti, meza na madawati kwa shule 23 mikoani humo, ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka sababu wanakaa katika mazingira mazuri wakiwa madarasani ambayo yamepelekea mahudhurio yao kuongezeka kwani wanafurahia elimu.

Pamoja na hilo, NMB imeendelea kutoa vifaa vya kuezeka katika shule (23)ambayo  imepunguza wanafunzi kubanana katika chumba kimoja na hivyo kusoma kwa nafasi bila bugudha.

Misaada hii imewanufaisha walimu, “Tumekuwa wanufaikaji wakubwa na uwajibikaji huu, kwani sasa kila mwalimu anafanya kazi yake kwa moyo mmoja na kuhakikisha wanafunzi wanasoma na tunaufaulu mzuri” alisema Mwalimu Mkuu, Joyce Munyu wa Shule ya Msingi Majengo.

Uwajibikaji wa namna hii ni sehemu inayoifanya benki kuishi kauli mbiu ya ‘NMB Karibu Yako’ lakini pia kuwa kinara na bora Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages