April 28, 2022

WASHIRIKI JUMA LA ELIMU TABORA WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI IGUNGA

Wadau wa elimu toa ka Mtandao wa Elimu Tanzania wakizungumza na wanafunzi kwenye mikutano ya uhamasishaji elimu katika Maadhimisho ya Juma la Elimu, Wilaya ya Igunga.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akizungumza katika moja ya ziara zinazofanywa na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kutembelea shule anuai na kuzungumza na wanajamii kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, wilayani Igunga.


Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (katikati) na ujumbe wake wa wadau wa elimu wakiwasili katika Shule ya Msingi Igunga ikiwa ni moja ya ziara zinazofanywa na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, wilayani Igunga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, Denish Otieno (kulia) akizungumza katika moja ya ziara zinazofanywa na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kutembelea shule anuai na kuzungumza na wanajamii kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, wilayani Igunga.

Wadau wa elimu wakizungumza na wanafunzi kwenye mikutano ya uhamasishaji elimu katika Maadhimisho ya Juma la Elimu, Wilaya ya Igunga.

Mikutano hiyo ikiendelea Maadhimisho ya Juma la Elimu, Igunga katika shule anuai.

Meneja wa Miradi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Alistidia Kamugisha (kulia) akizungumza na wanafunzi kwenye mikutano ya uhamasishaji elimu katika Maadhimisho ya Juma la Elimu.


Mkutano kati ya walimu wa Shule ya Msingi Igunga na wadau wa elimu wakiwemo wawanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania walipoitembelea shule hiyo kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu.

Afisa Program HakiElimu, Bi. Benedicta Mrema (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nanga wilayani Igunga kwenye mikutano ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa inayoendelea wilayani Igunga.

Mkutano kati ya wanafunzi limu wa Shule ya Msingi Igunga na wadau wa elimu wakiwemo wawanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania walipoitembelea shule hiyo kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu.

Mkurugenzi wa Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia, Dkt.Magreth Matonya akizungumza na wadau wa elimu, wanajamii, walimu, wanafunzi pamoja na wanachama wa TEN/MET Shule ya Msingi Igunga, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu, Igunga.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akizungumza katika moja ya ziara zinazofanywa na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, wilayani Igunga.

Ofisa Mawasiliano wa Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi (kulia) akiendesha majadiliano kati ya wanajamii na wadau wa elimu toka Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu, Igunga.

Wazazi na wazee maarufu wakiwa katika mkutano na wadau wa elimu na wawanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania walipoitembelea Shule ya Msingi Ganyawa kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu.


Mkutano kati ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanzugi na wadau wa elimu na wawanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania walipoitembelea shule hiyo kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu.

WASHIRIKI wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamefanya ziara kutembelea shule za msingi na Sekondari huku wakifanya mikutano ya kutoa elimu kwa wanajamii, wanafunzi, waalimu na wadau wengine muhimu katika elimu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya juma la elimu 

Wadau hao wa elimu na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) ambao wanashiriki katika Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa wilayani Igunga, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge wilayani Igunga, walifanikiwa kuzitembelea Shule za Msingi Igunga, Mwanzugi, Ganyawa pamoja na Shule ya Sekondari Nanga zote zikiwa wilayani Igunga.

Ziara hiyo zilizoshirikisha viongozi wa Serikali sekta ya elimu zilikwenda sambamba na wanachama wa TEN/MET kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuchangia uboreshaji wa elimu nchini, kuhamasisha na kukumbusha jamii, serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau mbalimbali wa elimu kuhusu umuhimu wa kuchangia elimu kwa ujumla.

Aidha wadau hao walifanikiwa kufanya mikutano ya uhamasishaji elimu katika makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo, walimu, wazazi, wanafunzi, viongozi wa madhehebu na wazee maarufu pamoja na wazee wa kimila lengo likiwa ni kuhamasisha kuboreshaji miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kwa kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama watoto wenye ulemavu na watoto wa kike. 

Zaidi ya mashrika yasiyo ya kiserikali 39 yenye wajumbe takribani 111 na Halmashauri yameshirikiana kuandaa maadhimisho ya mwaka huu, huku wakilenga kutatua changamoto za elimu Wilayani Igunga. Hii ni pamoja na kupanga mikakati endelevu ya kuondoa kabisa changamoto za uhaba wa madarasa, walimu, madawati, vyoo vya wanafunzi na walimu, pamoja na nyumba za walimu. 

Baadhi ya Mashirika wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania ni pamoja na Uwezo Tanzania, HakiElimu, Brac Maendeleo, REPSI, ADD International, ShuleDirect, Sense International, Malala Fund, WOWAP, Right to Play, CAMFED, WeWorld, Shule Bora, CASEE, AMUCTA, Pestalozzi Children’s Foundation, SAWO, CDO, Education Opportunity, Room to Read, Plan International, Lyra in Africa na Feed the children.

Wengine ni; KCBRP, CBIDO, KESUDE, KARUDECA, DRS, Beyond Giving, Mama Kevina Hope Children Centre, SALVE Regina, SMD, AWPD, Caritus Rulenge, Brothers of Charity, EOTAS, NELICO, MDREO, Sengerema CDH, Lake Victoria Disability Centre, St. Justin Center for Child with Disabilities, Children in Crossfire, Room to Read, AFRIWAG naTEN/MET Secretariat.

No comments:

Post a Comment

Pages