April 20, 2022

WAZIRI MBARAWA ATEMA CHECHE KUHUSU UJENZI WA DARAJA LA MTO WAMI

 


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawe wa (kulia) akigagua mradi wa ujenzi wa daraja la mto wami ambalo limejengwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 75.1 kushoto kwake ni balozi wa china nchini Tanzania Mingijian Cheni alipofanya ziara ya kukagua mradi huo.

 

NA VICTOR  MASANGU, PWANI

 

SERIKALI imesema kwamba kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi na daraja jipya la mto wami Julai  mwaka huu kutakuwa ni mkombozi mkubwa wa kupunguza wimbi la vifo kwa wananchi ambavyo vimekuwa vikitokana mara kwa mara  kutokana na kukithiri kwa changamoto ya kutokea kwa  ajali za barabarani kutokana na kuwepo  kwa miundombinu finyu katika daraja hilo la zamani.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ambapo amemuagiza  mkandarasi  wa Power  Construction kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo mwezi Juni mwaka huu badala ya  mwezi  novemba  21 mwaka huu kama ilivyokuwa  katika mkataba.

Pia waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi Power Construction kukamilisha ujenzi wa Daraja la Mto Wami ifikapo Juni badala novemba mwaka huu ambapo daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 75.1 mara litakapo kamilika.

 

Aliyasema hayo jana kwenye ujenzi wa Daraja hilo jipya lililopo Wami-Chalinze Wilayani Bagamoyo ambapo aliambatana na Balozi wa nchi ya China Ming Jian Chen na kuwa angependa arudi Juni 15 na kupita na gari kwenye daraja jipya na siyo la zamani.

 

Mbarawa alisema kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutasaidia kuokoa maisha ya watu ambao walikuwa wakipoteza maisha pamoja na mali kuharibika kutokana na ufinyu wa barabara hiyo kwani magari hayawezi kupishana tofauti na daraja jipya ambalo litakuwa na urefu wa mita 500.

 

"Daraja la zamani limejengwa mwaka 1959 ni jembamba na ni la njia moja ningefurahi kuona muda mliopanga kukamilisha Julai usifike mmalize Juni ijapokuwa mwanzo ilipangwa kukamilika Novemba mwaka huu kwani watu wengi wamekuwa wakipata shida kwenye daraja la zamani,"alisema Mbarawa.

 

 

Kwa upande wake Balozi wa china nchini Tanzania amesema kwamba wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika miradi mbali mbali ya maendeleo na kwamba daraja hilo la mto wami litasaidia kupunguza kasi ya ajali kwa  wananchi  mbali mbali  wa Dar es salaam, Pwani pamoja na nchi nyingine za jirani.

Aidha balozi huyo alifafanua kuwa mradi huo wa Maendeleo unaunganisha Mji wa Kibiashara wa Dar es Salaam na mikoa ya Kaskazini na kuleta maendeleo na nchi yake itaendelea kushirikiana bega kwa began a serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbali mbali ya ya maendeleo.

 

Naye Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANRODS) Injinia  Hussen Mativila amebainisha kwamba  mradi wa daraja hilo ambalo lina urefu wa mita 5.15  limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 75.1 na kwamba daraja la zamani ni chakavu na nifinyo  kutokan ana na magari kupita kwa shida kwani limejengwa tangu manamo  mwaka 1959.

Kadhalika mtendaji huyo mkuu wa Tanrods alisema kuwa mradi huo unagharimiwa na serikali na unatumia Teknolojia ya madaraja marefu kuna nguzo nne ambapo mbili zina urefu wa mita 19 nyingine ikiwa na urefu wa mita 37 na huku moja ikiwa na urefu wa mita 44.

 

No comments:

Post a Comment

Pages