April 22, 2022

WEKEZA UTT AMIS UPATE FAIDA MARA DUFU

 BAADHI ya Wajasiriamali wanachanganya dhana nzima ya kuweka na kuwekeza. Kimsingi maneno haya ni tofauti. Kwa mfano fedha zikiwa kwenye akaunti za akiba benki au kwenye kibubu nyumbani huko tumeziweka.

 

Lakini zikiwa kwenye akaunti ya muda maalumu benki tunasema zimewekezwa, pia tukinunua hisa au hati fungani za Serikali au kampuni binafsi zinakuwa zimewekezwa. Kulima mazao ya kibiashara kwa ajili ya kuuza kwa faida, kufuga kuchimba madini kwa ajili ya kupata na kuuza kwa thamani ya juu zaidi pia ni uwekezaji.

 

Uwekezaji mara nyingi huwa kuna faida, lakini wakati mwingine kuna hasara. Wapo wanaogopa kuwekeza kwa kigezo kuwa wanaweza kupata hasara. kuweka fedha mara nyingi huwa ni kwa ajili ya matumizi ya kila siku na kuzichukua kwa matumizi huwa ni rahisi.

Makala haya yanakusudia kutoa msukumo katika uwekezaji, wabobezi kwenye sekta ya uwekezaji wanashauri kwamba ni lazima pia kuweka kiasi fulani cha pesa ambacho kinaweza kutumika kipindi chochote hata kama itapungua thamani wakati wa mtikisiko wa uchumi.

 

Kuwekeza ni pale, ambapo unatumia fedha  au mtaji wako kununua rasilimali ambayo umetathmini kuwa itakupa kipato kizuri siku zijazo hata kama kutakuwa na changamoto.

 

Kuwekeza kunaweza kuwa kwenye masoko ya mitaji, dhamana mbalimbali, majengo, kilimo na viwanda.

 

Niweke na kuwekeza kiasi gani

Ukiangalia kwa undani dhana mbili utabaini kuwa fedha ya kuweka inatakiwa itoke kwenye faida ya rasilimali iliyowekezwa, hivyo inabidi kulitambua kama msingi wa ndoto za kuwa vizuri kiuchumi.

 

Kwa mfano kama ulirithi fedha nyingi, vinginevyo kile unachotenga kando, au utakachokopa ndio kitakupa nguvu ya kuwekeza na kukuza uwekezaji wako.

 

Watu wengi kwa sababu ya kukosa mitaji ni vizuri kutenga sehemu ya vipato na kuviweka sehemu, ambapo tunapata nafasi ya kuvipa vikiwa vimekuwa na sehemu salama zaidi ni  UTT AMIS.

 

Pia unaweza  kufikiria akaunti za muda maalumu, hisa au hata hati fungani la muhimu ni kupata mtaalamu akushauri jinsi ya kuanza hata kwa mtaji mdogo kama vile UTT AMIS ambapo unaweza kuanzia Sh. 10,000.

 

Kiasi hicho pekee huweza kukuza myaji kupitia Uwekezaji wa Pamoja, Ieleweke kwamba Serikali ilipoanzisha Uwekezaji wa Pamoja ilikuwa na nia ya kumwezesha Mtanzania hata yule mwenye kipato cha chini kabisa kuwa mwekezaji.

 

Kanuni ya kawaida ya kuweka inataka kile ulicho weka kitoshe kulipa gharama za kila siku zamaisha yako binafsi yakiwemo madeni, bima, gharama za maji, umeme n.k, chakula, malazi, nguo walau kwa miezi sita. 


Dhumuni ambalo malengo yake ni kuanzia miaka mitano na kuendelea linatakiwa liwe kama uwekezaji, lakini chini ya miaka mitano itakuwa ni kuweka. 

 

Hii ni kwasabu katika muda mfupi tukichukila hisa kama kigezo zaweza kuwa zimeporomoka hivyo basi muda kuhitajika ili zikuwe tena na hata zilete faida nzuri. 

 

Katika hali ya kawaida ukimudu gharama za kawaida za maisha na kuweza kujiwekea bima ya afya unakuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mwekezaji.

 

Ili tufanikiwe kimaisha na ili kuwekeza mfano kwenye mifuko ya Uwekezaji ya UTT AMIS ni lazima matumizi yetu yawe madogo kulingana na vipato vyetu. 

 

Yaani kama kipato chako ni shilingi laki tano kwa mwezi inabidi matumizi yako yawe shilingi laki nne kwa mwezi.

 

Majibu ya swali niweke au niwekeze ni kwamba hilo, litategemea na lengo au malengo yako na ukwasi ulio nao.

 

Kuweka kama nilivyosema ni kutenga kiasi kama ule msemo haba na haba hujaza kibaba kwa ajili ya mahitaji maalumu kama kwenda mbuga za wanyama, ulaya, nakadhalika. 

 

Wakati mwingine tunaweka kwa ajili ya kukabiliana na dharura zinazoweza jitokeza hapo baadae, na pesa kama hizi tunaziweka nyumbani au benki lakini kuwekeza tunaweka katika rasilimali ambazo zitatupa thamani kubwa zaidi baadae.

 

Jitahidi kuweka fedha yako kadri unavyoweza na hii imerahisishwa pale UTT AMIS kwani unaweza weka fedha zako kupitia simu yako ya kiganja, hii ina maana ya kuwa kabla hujafanya matumizi yeyote yale utajiuliza kama matumizi hayo ni ya lazima au laa. 

 

Ukipata jibu sio ya lazima utawekeza kwa njia ya simu au tawi lolote la CRDB au ofisi yeyote ya UTT AMIS.

 

Kwa simu ya mkono ni rahisi na ni masaa 24, siku 7 za wiki. 

 

Swali ni je, uko tayari kuwekeza?

 

Nenda UTT AMIS uzungumze nao kuna mifuko ya uwekezaji yenye malengo mbalimbali, mfano; 

 

UMOJA-Kukuza mtaji 

 

WEKEZA MAISHA-Huduma za Bima na kukuza mtaji.

 

WATOTO-Ada za shule au mtaji kwa matoto amalizapo shule.

 

JIKIMU-Gawio la mara kwa mara.

 

UKWASI-Kipato cha wastani katika muda mfupi.

 

Uwekezaji wa muda mfupi na kati kwa faida inayoendana na riba za mikopo katika hati fungani.

 

Kwa mipango ya muda mfupi  waweza weka au wekeza katika benki kwa maana ya katika akaunti za muda mfupi na muda maalumu.Pia katika hati fungani za mwaka mmoja na katika benki kupitia mikopo ya muda mfupi.

 

Muda wa kati na muda mrefu yaani Zaidi ya miaka 5 unaweza wekeza katika hati fungunani na katika hisa Ni muhimu kuzingatia mfumuko wa bei kwani shilingi ya leo itanunua vitu vichache siku zijazo- katika hali ya kawaidi.

 

Zaidi ya mfumuko wa bei angalia faida tarajiwa, usalama, na urahisi wa kupata pesa zako zote au kiasi pale unapozihitaji.

 

Uwekezaji unatakiwa uwe kitu ambacho hakifi, yaani sisi tuliowekeza tuage Dunia  na wanao tuhusu wachukuwe usukuni mpaka nao waondoke wakiwaachia wanao wahusu, mfano wa kampuni kama Toyota, Ford, Apple walio anzisha hawapo tena Duniani tena miaka mingi lakini zenyewe zinazidi kushamiri. 

 

Hisa ni sehemu nyingine nzuri sana kwa mtu mwenye lengo la muda mrefu na hata kuacha urithi wa milele. Uwekezaji katika hisa au mchanganyiko wa masoko ya mitaji na dhamani ndio kazi ya UTT AMIS chukuwa hatua kawaone wakupe mwanga Zaidi.

 

Pia unaweza kwenda soko la hisa Dar es Salaam, kwa madalali wote wa soko la hisa, benki zote, na kwa mamlaka ya kusimamia masoko ya hisa na mitaji.

 

Kama tunavyofahamu mtu akiwa na kiasi cha pesa kwa kiwango fulali hivi, kwa mfano wa shs 5,000,000 UTT AMIS mfuko wa Umoja kwa miaka 16 imekuwa shs 55,000,000 hivi. Hizi shs 5,000,000 zingekuwa ziko ndani tu zingekuwa zinapoteza thamani kwa walau aslimia 4 kila mwaka na katika akaunti za akiba za kawaida  thamani ingekuwa inashuka si chini ya asilimia 2. Na kwa uzoefu hizi shs 55,000,000 zitakuwa zinakuwa mara dufu kila miaka 5 hivi.

 

UTT AMIS ni Kampuni ya uwekezajia wa pamoja ya taifa iliyo chini ya Wizara ya Fedha. Kazi kubwa ya UTT AMIS ni kubuni na kusimamia mifuko ya uwkezaji wa pamoja. Mpaka sasa kampuni hii inasiammia mifuko 6,  kwa majina Umoja, Wekeza      Maisha, Watoto, Jikumu  na Ukwasi.

 

Mifuko yote hii imekuwa ikitoa faida nzuri kwa wawekezaji wake japo mwendo wa kipande umekuwa ukipanda na wakati mwingine kushuka kwa mfano bei ya kipande cha Umoja (2005) ni karibia shilingi 810 kwa sasa ikilinganishwa na shs 70 mfuko ulipoanza.

 

Wekeza maisha (2007) ulianza kipande kikiwa shs 100 lakini leo hii bei ya kipande ni shilingi 682, kipande cha mfuko wa Watoto (2008) kwa sasa una karibia thamani ya shilingi 504 lakini ulianza kwa shilingi 100.

 

Jikimu (2008) ulianza kwa shilingi 100 lakini sasa unakaribia shilingi 151 pamoja na ukuwaji huu mfuko huu umekua ukitoa gawiwo la asilimia 12-16 kwa kila mwaka tokea kuanzishwa.

 

Ukwasi (2013) ulianza kipande kikiwa shilingi 100 lakini miaka 8 tokea kuanzishwa kipande sasa kinakaribia shilingi 313 . Kwa maana nyingine, safari ya kipenda ni kama safari ya binadamu kwani hupita katika milima na mabonde, wakati mwingine kwenye mifereji na mito. Lakini pamoja na yote hayo uwekezeji kupitia UTT umekuwa ukitoa faida nzuri ukilinganisha na uwekezaji fananishi, katika masoko ya hisa na masoko ya fedha.


Mfuko wa hati fungani umekuwa ukitoa gawio la asilimia 1 kila mwezi au Zaidi ya asimia 6 kila miezi sita huku thamani ya kipande chake ikiwa imekuwa anzia shilingi 100 (2019) mpaka shilingi 115 (April 2022).

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages