May 13, 2022

BENDI ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO TAMASHA LA USIKU WA WAFIA DANSI JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa  Bendi ya muziki wa Dansi ya Waluguru bendi , Kill Boy (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu bendi yake kushiriki katika kutoa burudani katika tamasha hilo litalofanyika Tarehe 28 mwezi huu  jijini Dar es Salaam kulia ni Rais wa Bendi ya Mjengoni Classic, Digital Mukongya,

Muandaaji wa Tamasha la Usiku wa Muziki wa Dansi lijulikanalo kwa jina la usiku wa Wafia Dansi, Benard James (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kufanyika tamasha hilo Tarehe 28 mwezi huu jijini dar es Salaam, kulia ni Rais wa  Bendi ya Mjengoni Classic, Digital Mukongya, na (katikati) ni Rais wa  Bendi ya Waluguru, Kill Boy,

 

Na Dotto Mwaibale

 

BENDI tano zinazopiga Muziki wa Dansi nchini, Mei 28, mwaka zitawasha moto kwenye Tamasha la Wafia Muziki wa Dansi linalotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Gwambina, zamani TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. 

 

Akizungumza Jana na waandishu wa habari, Mratibu wa tamasha hilo, Bernard James kutoka Kampuni ya Cheza Kidansi Entertainment ambao ndiyo wadhamini anesema lengo la tamasha hilo ni kuufufua muziki wa dansi ambao haupewi kipaumbele nchini. 

 

James amezitaja bendi zitakazoshambulia jukwaa kwa pamoja kuwa ni bendi ya Mapacha Music Band inayoongozwa na Jose Mara, Bogoss Music chini ya Nyoshi el Sadaat Musondo Ngoma Music Band zote za jijini Dar es Salaam. 

 

Aliongeza kutakuwa na bendi mbili kutoka nje ya Dar es Salaam ambazo ni Waluguru Original ya Morogoro na Mjengoni Classic ya Arusha.

 

"Huu muziku wa dansi una  mashabiki wengi ndani na nje ya nchi Ni vyema uendelezwe ili vizazi vijavyo vije vifahamu nyimbo zenye meseji nzuri  na maadili ya kitanzania," alisema James. 

 

Aliongeza Wizara ya utamaduni, Sanaa, Michezo na Chama Cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) vihakikishe vinaupa kipaumbele muziki huo kwa lengo la kuuendeleza. 

 

"Muziki wa Dansi unahistoria na mchango mkubwa si Tanzania tu Afrika kwa ujumla, wakati wa kupigania Uhuru ulitumika sana," alisema. 

 

Kiongozi.na mwimbaji wa Bendi ya Mapacha, Jose Mara amesema siku hiyo anatarajia kutoa burudani nzuri kwa wadau was muziki na mashabiki wake ambapo atautumia usiku wa Tamasha Hilo kuzindua nyimbo zake mbili zinazoitwa Nitakuwa Sawa.na Hukumu ya Mapenzi. 

 

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Green International ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, Kessa Mwambeleko alitoa wito kwa wadau wa muziki wa Dansi nchini kujitokeza kwa wingi kusaidia kuuendeleza muziki huo ili uwe na mashabi wengi Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. 

 

Mwambeleko aliongeza  kuwa kampuni yao inayojuhusisha na usambazaji wa pembejeo za kilimo na viutalifu imeamua kudhamini tamasha hilo ili kuwapa burudani wakulima ambao ndiyo wadau wao. 

 

Natoa rai kwa wapenzi wa burudani ya muziki wa dansi wa jijini Dar na mikoa jirani wajitokeze kwa wingi pale kwenye ukumbi wa Gwambina zamani TCC Chang'ombe Temeke kwenye Tamasha la Wafia Muziki wa Dansi wataburudika kwa muziki utakaoporomoshwana bendi shiriki," alisema Mwambeleko. 

 

Alitaja viingilio vitakuwa ni Shilingi 10,000 kawaida na VIP Shilingi 30,000.


No comments:

Post a Comment

Pages