May 30, 2022

ELIMU SI HESABU ZA DARASANI TU TUWAFUNZE WATOTO ELIMU DUNIA PIA

Kama wazazi tunapaswa kufahamu kuwa hesabu za darasani hazitoshi kama elimu pekee kwa watoto. Kama wazazi tuna wajibu wa kufanya kila jitihada kuhakikisha watoto wetu wanakuwa werevu wenye elimu zaidi ya ile ya darasani.  Tunataka wawe na msingi imara kwa maisha yao yote.

Ili wapate maisha ya furaha ni lazima wawe na uchumi mzuri, na uchumi hupimwa na kiasi cha mali, mali kuu ikiwa ni pesa na pesa hupatikana kwa maarifa huku elimu ya darasani ikisaidia tu kwenye utafutaji, kwani wapo wenye pesa nyingi lakini walikimbia umande.

Elimu ndiyo silaha kubwa kuliko zote inayoweza kutumika kubadilisha dunia – Nelson Mandela. Elimu inasaidia kupata maarifa, ufikiri wa kina ndani ya misingi imara, na hutupa maarifa ya kubuni nyenzo zenye kurahisiha maisha. Na hapa haina maana elimu ya darasani tu.

 Yeyote atakaye simama kusoma ni mzee, haijalishi umri wake. Kuwekeza kwenye elimu kuna lipa na sababu uwekezaji wote unahitaji pesa basi elimu ya pesa yapasa kupewa kipaumbele.

Bila elimu ya pesa maisha yaweza kuwa magumu, na kwa sbabu vijana ni asilimia kubwa ya watu duniani, ufukara hutanda wasipo funzwa mambo mbali mbali. Swali ni je tuna wafundisha watoto wetu?

Wakipata  elimu ya fedha, watafanya chaguzi nzuri za ni wapi wapeleke pesa zao. Na wataweza zitumia vizuri na kuepuka kuwa tegemezi kwa mtu ki-fedha.

Wakipata elimu mapema maana yake watakuwa na uhuru wa kifedha katika maisha yao yote.

Elimu ya fedha ina muwezesha mtoto kutofautisha fungu la matumizi ya lazima, yasiyokuwa ya lazima, na dharura. 

Tukumbuke maarifa yangekuwa ya kuendesha basikeli, gari au hata kuogelea yanakuwa rahisi yakiwa sehemu ya maisha ya mtoto angali mdogo. Hivyo basi nidhamu ya fedha nayo ina jijenga kwa wepesi n ahata kuwa tabia kama ikifundishwa kwa watoto wangali wadogo.

Pesa ni kila kitu, tunakula, tunavaam tunamapata malazi na tunapigana na maradhi ki urahisi kama tukiwa na pesa, bila pesa maisha yanakuwa magumu.

 Kama wazazi tunapaswa kufunza watoto wetu jinsi ya kutafuta, kutunza, na kutumia pesa. Wengi wetu tunahimiza shule tu, n ahata inapokuja juu pesa  tunasita kuzungumza na watoto wetu ‘ mimi nilitafuta zangu na wao watafute zao’ wengi tunasema hivyo lakini hatuwa ambii watafute vipi na pesa zetu mara nyingi zinakuwa si sehemu ya maisha yao zaidi ya kula, kuvaa na tiba. Pengine wanazipata kwa kurithi pale mauti yanapo tifika.

Tufanyeje? Anza mapema, kabla ya miaka saba kumfunza mtoto. Waambie pesa ni nini na matumizi yake ni yapi?  Mkienda dukani mpe japo elfu moja anunue kitu, na arudishiwe chenji, mfundishe jinsi ya kuhifadhi chenji kwa manunuzi mengine ya baadae ili ajuwe kuna leo na kesho. Kwa kujifunza kuweka kwa ajili ya kesho dhana ya fedha kuwa kwa ajili ya kutumia tu ita ondokana nao hivyo basi watengenezee kibubu, kama wako wengi acha washindane yupi atakuwa ameweka akiba kubwa zaidi ya mwenzake ndani ya muda Fulani . wanavyi zidi kukuwa watoe kwenye kibubu kwenda benki na baadae sehemu kaa vile UTT AMIS.

Kumbuka watoto wanatakiwa kuweka hela waliyo itafuta wao wenye, hivyo basi nikisema mpe sina maana mpe bure. Mpangie kusafisha banda la kuku kama lipo halafu mpe ujira, au mpe changamoto ya kuwa wa kwanza darasani akiifikia mpe. Kuna kazi kama vile kuosha magari ya nyumbani, kutengenza bustani ya  maua ya nyumbani na mambo mengine mbali mbali.  Lazima wafanye kazi Fulani ili kupata kipato.

Bila kuwapangia unaweza mwekea kila mmoja vibu viwili au vitatu. Kimoja kwa matumizi ya kila wiki na kigine kwa safari au jambo Fulani mwisho wa mwaka au ndani ya miaka Fulani ijayo. Wafundishe kutoa pia, kusaidia jamii. Na jichunge kauli zako huwezi kuwaambia watoto watunza hela halafu kila siku unatoka nao na mabunda ya pesa, huku mkinunua kila kivutiacho machoni. Tekeleza kwa vitendo lile uwafundishalo.

Hivyo basi, ni ndoto ya kila mzazi kuwa na mtoto mwenye Maisha mazuri na yenye furaha. Maisha mazuri yanachangiwa na mambo mengi, lakini pngine kubwa Zaidi ni elimu na ukwasi.Ukwasi ni ile hali ya kuwa una pesa, yaani unamuda gharama zako za Maisha za kila siku sababu mfukoni panakuwa hapa kauki. Ukwasi unaletwa na mabo mengi, waweza kuwa umerithi au waweza kuwa umetafuta au hata umepata bahati nasibu kubwa, yote haya yatakuwa na maana tu kama mtoto atakuwa na elimu ya kuwekeza, elimu ya pesa kwani hata kama karithi hela atakuwa amezi ridhi kwa wazazi au ndugu ambao waliwekeza hapo awali, pia ukipata bahati nasibu ni lazima ujuwe ni wapi utawekeza ili zizidi kukupa kipata au hata kukuwa Zaidi,

 

Kama una mototo ni muhimu kuanzia umri mdogo kabisa kuwapa elimu ya pesa, jinsi ya kutafuta pesa, jinsi ya kuzitumia na jinsi ya kuzitunisha ziwe nyingi Zaidi. Mtoto anatakiwa ajuwe vyanzo vya pesa, kuhifadhi fedha, bajeti, mikopo na athari zake na matumizi ya pesa. Kumbuka elimu na ushawishi watakao pata kutoka kwako ndio itakuwa ngao ya Maisha yao ya baadae.

 

Kwanini tuanze kuwafunza Watoto elimu ya uwekezaji na pesa, ni kwa sababu wao wanayo zawadi ambayo mimi na wewe hatuna, muda. Muda ni muhimu sana katika uwekezaji,

Mtoto akianza mapema atapata faida ya kukuza kipato n ahata kupata mtaji baade, au hata kupata hela ambazo zitampa hela ya kula kwa mpango wa gawio la kila mwezi mpaka uko wa maisha yake yote ya dunia.

 

Kwa mfano uwekezaji kupitia mifuko ya UTT AMIS ambayo hutoa faida jumuishi kwa uwekezaji mdogo mdogo tu kwa muda mrefu mtoto atakuwa amekuza kipato chake.

Mfano mtoto mwenye miaka 5 ukalimpa shlingi elfu 50 kwa kila mwezi kwa kufanya kazi za nyumbani  akiwa na miaka 25 ataweza kuwa na walau shlingi  milioni 50.5 kwa faida ya aslimia 1 kwa mwezi hii ikiwa faida ya shilingi milioni 38.4 kutoka kwenye uwekaji wa shilingi milioni 12 hivi katika muda huo.

Baada ya miaka 25 huyu mtoto ata anza kazi na hivyo basi ataweza kuwekeza shilingi 150,000 kwa mwezi ambazo kwa silimia hiyo hiyo ya faida kwa mwezi kwa miaka 20 ijayo atakuwa na miaka 45 huku akiwa amewekeza shilingi  milioni 36 hivi, faida ikiwa shilingi milioni 115 hivi na jumala ya pesa zake zikiwa shilingi milioni 151 hivi.

Kumbuka huu ni uwekezaji mdogo mdogo wa awali shilingi elfu 50 kwa mwezi na baada ya kupata kazi shilingi 150,000 kwa mwezi mpango wa kabla ya miaka 25 alipata shilingi 50 na mpango wa  baada ya miaka 25 alipata  shilingi milioni 150. Jumla ni shilingi milioni 200.

 

Mfano wa mwisho ni unapooanza kuwekeza kiasi cha shilingi 100,000 na kila mwezi baada ya hapo ukawekeza shilingi 100,000 kwa miaka 15 Jumla ya uwekezaji wako wa mwanzo na wa kila mwezi kwa muda huo utakuwa shilingi 18,000,000; iwapo riba ilikuwa ni asilimia 1 tu kwa mwezi. Uwekezaji wako na faida utakuwa  jumla shilingi 50,557,599 hii ina maana utakuwa umepata faida halisi ya shilingi 32,457,599 hii ndiyo maana ya faida jumuishi.  Sasa hiki ni kiasi cha shilingi 100,000 tu kwa mwezi je kama unaweza wekeza

Kama unaweza ongeza muda wa uwekezaji mfano mtoto alianza kuwekezewa akiwa na mwaka mmoja kiasi hicho hicho  na riba hiyo hiyo akiwa na miaka 30 atakuwa na shilingi 353,091,377, yaani hela ambazo zitakuwa zimetoka mfukoni kwa wazazi/mtoto ni 36,100,000 lakini kwenye uwekezaji atakuwa na shilingi  353,091,377  faida peke yake ikiwa shilingi 316,991,337 haya ndiyo maajabu ya faida jumuishi.

 

Ki ujumla vijana lazima waandaliwe vizuri wafahamu namna ya kutafuta mitaji, jinsi ya kuwekeza hiyo mitaji, umuhimu wa muda kwenye uwekezaji, kodi mbali mbali kwenye biashara, na mengine muhimu kama vile kutoweka mayayi yote kwa kapu moja. Waulize maswali kuhusu fasheni za nguo, viatu au mavazi kwa ujumla, biashara za vimiminika, chakula na hata usafiri, zipi ni za mtaji mkubwa na zipi zinahitaji mtaji mdogo.

Watoto wanapaswa kufahamu umuhimu wa kununua na kushikilia, kwa mfano ukinunua hisa au vipande, pia ukanunua kiwanja au shamba matarajio katika hali ya kawaida ni kuwa miaka kadhaa ijayo thamani ya ulicho kinunua itakuwa imepanda ten asana, na mara nyingi itakuwa imepanda na hata kukabili  hatari za vitu kama vile mfumuko wa bei. Na pia ni muhimu kuwaelimisha kuwa si kila wakati matarajio yao yatafikiwa kwani kwenye kuwekeza kua kupanda na kushuka.

 

Subira ni jambo lingine muhimu, busara na uvumilivu mwana falsafa mmoja kwa jina Albert Einstein aliseam faida jumuishi ni nguvu ya ajabu duniani, faida jumuishi ina uhusiano wa moja kwa moja na muda yaani muda  unavyokuwa mrefu huku ukiweka nidhamu ya kuacha mbegu na matunda vichanganyike Pamoja basi utafaidi sana kadri muda unavyo kwenda mfano ukiwekeza milioni 5 halafu ukawekeza shilingi laki 2 kila mwezi kwa miaka 10 wewe utakuwa umetoa kutoka katika mfuko wako shilingi milioni 29 lakini kwa asilimia 1 kwa mwezi utakuwa na Zaidi ya milioni 70, na ukafanya hivyo kwa miaka 20 wewe utakuwa umetoa shilingi milioni 53 toka kwa mfuko wako lakini utapata Zaidi ya shilingi milioni 360 ndani  ya hiyo miaka 20.

 

Wafunze kanuni ya 72, hii inafundisha ni  ndani ya muda gani pesa yako yaweza kukua mara mbili. Unachukuwa 72 unagawa kwa riba tarajiwa 72/riba. tuchukulie rib ani asilimia 7, ukigawa 72kwa saba utapata 10.28, hii 10.28 inamaanisha kama umewekeza sehemu kwa riba ya asilimia 7 itachukuwa miaka 10.28 pesa zako ziwe mara 2.

Mifuko  mingi ya UTT AMIS japo tunasema kipande kinaweza kupanda au kushuka inatoa riba wastani wa asilimia 13 hii ina maana kuwa 72 gawa kwa 13  ( 72/13 ) hii ina maana kuwa itachukuwa miaka 5.5 pesa zako kuwa mara mbili.

Tuchukulie mfano wa mfuko wa ukwasi ambao ulianza bei ya kipande ikiwa shilingi 100 na sasa bei iko shilingi 280 hii ina maana kuwa aliye wekeza shilingi milioni 100 leo ana shilingi milioni 280 ndani ya miaka 8. Mfuko wa ukwasi umekuwa ukilipa wastani wa asilimia 14; hivyo basi tukigawa 72/14 utapata 5.1 hii ina maana kuwa ndani ya miaka 5 hela ilishaongezeka mara 2 na  baada ya hapo kuna ongezeko la nukta 8.  Hii ni elimu muhimu kwa mtoto, kwani inampa uwezo wa walau kufahamu uwekezaji utakuwa mara dufu ndani ya muda gani.

 

Cha muhimu wafunze Watoto kuwekeza japo kidogo, watambue kuwa hata ukiwapa pesa kwa matumizi yao ni muhi watenge kiasi kidogo na kukiwekeza. Wakifanya hivyo watajenga utamaduni wa kuwekeza kwa ajili ya kesho yao. Tukiwa na wawekezaji wengi tunakuwa na familia na taifa bora. Jiulize unataka mwanao awe bwana matumizi au bwana mwekezaji?

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages