Mjiolojia Fortunatus Kidayi akitoa maelezo kuhusu mradi wa LNG kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab R. Telack aliyetembelea banda la PURA katika Maonesho ya Tano ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea mkoani Morogoro.
Na Ebeneza Mollel
Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeeleza kuwa imejipanga kikamilifu kusimamia mradi wa kubadili gesi asilia kuwa kimiminika (LNG) ili kuhakikisha mradi huo unaleta tija na kuchangia maendeleo ya uchumi nchini.
Hayo yamesemwa na Mjiolojia Fortunatus Kidayi alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab R. Telack aliyetembelea banda la PURA katika Maonesho ya Tano ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea mkoani Morogoro.
Alifananua kuwa miongoni mwa majukumu ya PURA kwa mujibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 ni kusimamia mradi wa LNG. Mradi huu unalenga kuvuna gesi asilia iliyogunduliwa kina kirefu cha bahari nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani na kiasi kingine kuuzwa nje ya nchi.
“Mradi huu ni wa thamani ya Dola za Marekani bilioni 30 na unatarajiwa kutekelezwa eneo la Likong'o mkoani Lindi na PURA imeendelea kujiimarisha kiutendaji ikiwemo kuendelea kuwajengea watumishi wake uwezo katika eneo la LNG" alieleza Bw. Kidayi.
Aliongeza kuwa PURA imejipanga kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kushiriki katika mradi wa LNG kupitia ajira na utoaji wa huduma na bidhaa katika kipindi chote cha utekelezaji wake.
“Katika kufanikisha hilo, PURA kwa kushirikiana na EWURA imeandaa kanzi data ya kuwasajili watoa huduma wa Kitanzania na wazawa wenye taaluma mbali mbali ikiwemo masuala ya mafuta na gesi. Kanzi data hiyo inajulikana kwa jina la Common Qualification System (CQS) na iko tayari kutumika,” alibainisha.
Aliongeza kuwa “mradi wa LNG unatarajiwa kuleta fursa nyingi nchini ikiwa ni pamoja na ajira zaidi 6,000 na ikiwa ni pamoja na fursa za kuuza bidhaa na huduma wakati wa utekelezaji wa mradi huo. Serikali ilishatoa Shilingi bilioni 5.7 kulipa fidia kwa wananchi zaidi ya 640 waliopisha utekelezaji wa mradi. Aidha, majadiliano baina ya Serikali na kampuni zitakazotekeleza mradi wa LNG yanaendelea na yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni".
Kwa upande wake, Mhe. Telack ameipongeza PURA kwa kusimamia suala ushiriki wa Watanzania kwenye shughuli za mkondo wa juu wa petroli, na kusema kuwa wananchi wa mkoani humo wanasubiri kwa hamu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na kwamba ana imani watapewa kipaumbele wakati wa utekelezaji wake.
ENGLISH
PURA EXPRESSES ITS PREPAREDNESS TO OVERSEE THE LNG PROJECT
By Ebeneza Mollel
The Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA) has expressed its readiness and commitment to oversee the upcoming liquefied natural gas (LNG) project and ensure the project is productive and contributes to the country's economic development.
This was stated by Geologist Fortunatus Kidayi while briefing the Lindi Regional Commissioner, Hon. Zainab R. Telack who visited the PURA pavilion at the Fifth Exhibition of Funds and Economic Empowerment Programs taking place in Morogoro region.
He explained that one of the responsibilities of PURA in accordance with the Petroleum Act of 2015 is to oversee the LNG project. This project aims to harvest natural gas discovered in the deep sea in Tanzania for domestic use and exports.
"This project is worth around USD 30 billion and is expected to be implemented in Likong'o area in Lindi region and PURA has continued to strengthen itself practically including continuing to build the capacity of its staff in the LNG area" said Mr. Kidayi.
He added that PURA is committed to ensuring that Tanzanians get the opportunity to participate in the LNG project through employment and service delivery throughout its implementation.
“In achieving this, PURA in collaboration with EWURA has developed a Common Qualification System (CQS) which will contain database of Tanzanian service providers and professionals, including those who studied oil and gas courses and that the system is already working,” he noted.
He added that “the LNG project is expected to bring many opportunities in the country including more than 6,000 jobs and including opportunities to sell goods and services during the implementation of the project. He further explained that the government has provided 5.7 billion shillings to compensate more than 640 citizens who will be affected by the project. In addition, negotiations between the Government and the companies that will implement the LNG project are ongoing and are expected to be completed soon."
For her part, Hon. Telack commended PURA for overseeing the issue of Tanzanians' participation in the petroleum upstream activities, saying that Lindi citizens are eagerly awaiting the start of the project and that she is confident they will be given priority during its implementation.
No comments:
Post a Comment