May 10, 2022

Taasisi za dini zatakiwa kusaidia jamii

Mchungaji Kiongozi wa  kanisa la Talitha Cumi Daniel Kitua,wakati akihubiri injili jumapili iliyopita kanisani hapo.

Diwani wa Kata ya Tambukareli Jiji la Dodoma Juma alipokuwa anazungumza na viongozi wa kanisa hilo.

 

Na Kadala Komba, Dodoma

TAASISI za kidini na wadau wa maendeleo wamekumbushwa kuzisaidia jamii zisizojiweza ikiwemo katika nyanja mbalimbali kama vile ya kiafya, kielimu, chakula, mavazi na uchumi ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha.


Ushauri huo umetolewa na Mwangalizi wa kanisa la Talitha Cumi Daniel Kitua,wakati alipokuwa akikabidhi kadi za bima za afya kwa watu wasiojiweza wapatao 75 wakiwemo wazee wasiojiweza na wenye ulemavu kutoka kata ya Tambukareli Jijini Dodoma.


Kituo alisema kuwa taasisi za kidini na wadau wa maendeleo wanawajibu wa kusaidia jamii hiyo isiyojiweza badala ya kuona suala hilo ni la serikali peke yake na wafadhili wa kutoka nje ya nchi.


Alisema kuwa kadi hizo la bima ya afya zilizotolewa na kanisa hilo zimelenga kuwasaidia katika kupunguza gharama wa kupata matibabu kwenye  vituo vya afya vinavyotoa huduma za kiafya.


“Kanisa la Talitha Cumi,limeona liwasaidia wazee hao na watu wanaoishi katika mazingira magumu kadi za bima ya afya,ili kuwapunguzia gharama kubwa ya matibabu pale wanapokwenda kupata matibabu kwenye vituo vya afya.alisema.
 

Kwa upande wake diwani wa kata ya Tambukareli Jiji la Dodoma Juma Mazengo,alisema kuwa serikali bado inadhamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi kidini na wadau wa maendeleo kwa kuhakikisha wanaisaidia katika kutoa misaada yake kwa jamii isiyojiweza.

 
Mazengo alisema kuwa kitendo kilichofanywa na kanisa la Talitha Cumi kinatakiwa kuigwa na taasisi zingine za kidini ili ziweze kuwafikia walengwa walio wengi ambao wana wanakabiliana na maisha magumu kila siku.


Naye mdau wa maendeleo Elice Yohana akizungumza na waandishi wa habari,alisema kuwa  msaada huo utasaidia kwa wasiojiweza,kuokoa afya na maisha yao.


Alisema bado kuna ulazima wa kuwaangalia jamii hiyo yenye uhitaji,ili wafikiwe na waweze kuondokana na kero wanazozipata kama vile kwa upande wa afya,elimu,chakula na mavazi.

 
Awali akihubiri kwenye ibada hiyo ya kukabidhi kadi za bima ya afya iliyofanyika katika kanisa la Talitha Cumi jijini Dodoma,Askofu Mkuu wa huduma ya The Word of Prophec Ministry Tanzania Proff John Mwakilemi.
 

Amewakumbusha Watanzania kuwa na umoja na upendo kwa ajili ya jamii isiyojiweza ili waweze kujikomboa na changamoto zinazowakabili iliwemo suala zima la kiuchumi na afya.

 
Prof Mwakilemi alisema kuwa Watanzania wakiwa na upendo na umoja utaweza kuwakumbua jamii hiyo,ambayo inakutana na changamoto nyingi wanazotaka zitatuliwe kwa upande wao.

No comments:

Post a Comment

Pages