May 14, 2022

SERIKALI YAIAGIZA TAASISI YA ELIMU KUNUNUA MASHINE YA KUCHAPA VITABU VYA NUKTA NUNDU

   

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akikaribishwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba wakati wa ziara ya kutembelea viwanda vya kuchapa vitabu jijini Dar es Salaam.

  

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchapa vitabu na machapisho mbalimbali kinachosimamiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),  John Kaswalala wakati wa ziara ya kukagua viwanda vinavyosimamiwa na taasisi hiyo. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akiangalia kazi zinazofanywa na Kiwanda cha kuchapa vitabu cha Press A, wakati wa ziara ya kukagua viwanda vya vitabu na machapisho mbalimbali vinavyosimamiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho, John Kaswalala.  

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akiangalia machapisho ya nukta nundu alipotembelea kiwanda Press B cha kuchapa vitabu vya wasioona. Kulia ni Meneja wa Kiwanda hicho, Adonia Mpemba.


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema Serikali inatumia shilingi bilioini 15 kila mwaka kuchapisha vitabu vya nukta nundu vinavyotumiwa na wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu.


Hiyo inatokana na malighafi ya karatasi inayotumika kuchapia vitabu hivyo kutopatikana nchini na badala yake kuagizwa kutoka Dubai na Marekani.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema fedha hizo ni nyingi ambapo ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuweka mkakati ndani ya mwaka mmoja iwe imepata mashine kubwa ya kuchapa na kutafuta tenda nafuu ya malighafi ya karatasi.


Mkenda ameyasema hayo leo Mei 14, 2022 katika ziara yake ya kukagua viwanda vya viabu na machapisho mbali mbali vinavyosimamiwa na TET.

"Dubai ni Jangwani, hakuna miti Waka hawazalishi karatasi, sisi tunaenda kuchapa huko kwa fedha nyingi, nataka na sisi tukanunue malighafi huko wanakonunua wao tuchapishe wenyewe."Amesema Mkenda na kuongeza

"Wafadhili wanaotupatia fedha masharti tenda ya kuchapa itangazwe kimataifa, sasa badala sisi tutangaze tenda ya kuchapiwa bora tutangaze tenda ya kupata mashine kubwa ya kisasa hii itapunguza gharama." Amesisitiza

Amesema mashine kubwa zaidi ya uchapaji huuzwa shilingi bilioni  30, hivyo watazungumza na wafadhili kuwaeleza wafanikishe hilo, kwani wanatekeleza manunuzi ya kimataifa ikiwa ni moja ya sharti la wafadhili hao.

Lakini, wataangalia inagharimu kiasi gani kuchapa Tanzania na inalinganaje kimataifa ikiwezekana serikali itakopa  katika taasisi za kimataifa na kuendelea kuchapa nje.

Amesema changamoto baadhi ya mitambo haiko 'automated'.

Kuhusu kuihusisha sekta binafsi, amesema ni vigumu kufanya hivyo kwa kuwa inachukua muda mrefu kupata faida.

"Wenyewe wangechangamkia iwapo kungekuwa na faida ya haraka, lakini wanaangaza kuchapa wao ili kuishawishi sekta binafsi." Amesema

Aidha, Mkenda amesema  serikali imedhamiria kuimarisha uchapishaji kwa kuiwezesha TET kupata karatasi kwa bei nafuu, umeme wa uhakika na mashine kubwa ya kisasa ya uchapaji.

Kupitia fedha za Covid 19 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu imewezesha TET kuchapa  vitabu vya nukta nundu vyote vya kidato cha kwanza hadi cha sita.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TET Dk. Aneth Komba akizungumza awake amesema sababu ya kutochapa nchini ni gharama kubwa ya karatasi, kutokuwepo kwa umeme wa uhakika na wa bei nafuu na mitambo ya kutosha kumudu uchapaji kulingana na mahitaji

Amesema Kiwanda cha uchapaji cha Magogoni ni moja kati ya viwanda saba vya taasisi hiyo na walikabidhiwa na wizara tangu mwaka 2019.

"So far kinatumika kuchapa muongozo wa walimu darasa la awali hadi la saba na kwa mwaka huchapa vitabu milioni tatu  ukihusisha na vya wenye uoni hafifu."Amesema

Amesema mahitajinya vitabu hivyo yanakidhi kwa mfano wenye uoni hafifu wastani wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu

No comments:

Post a Comment

Pages