May 12, 2022

TATHMINI YA ZIARA ZA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, NCHINI UGANDA NA MAREKANI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni, na Michezo Mhe. Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Uganda na Marekani kwenye Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Mei, 2022. (Picha na Ikulu).

 

1.    ZIARA NCHINI UGANDA:

 

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alifanya ziara yake ya kwanza ya Kiserikali nchini Uganda tarehe 10-11 Mei 2022, ambapo mafanikio mbalimbali yamepatikana kwenye ziara hiyo ya siku mbili.

 

Uhusiano na ushirikiano - Uhusiano wa kindugu na ushirikiano wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali baina ya Tanzania na Uganda umezidi kuimarika kutokana na kufanyika kwa ziara hiyo ambapo mambo mbalimbali yamejadiliwa na mikataba kadhaa imesainiwa kwa faida ya nchi hizi mbili.

 

Ukuaji wa biashara baina ya Tanzania na Uganda – Katika ziara hiyo, Uganda imeingia makubaliano kuiuzia Tanzania tani 10,000 za sukari ili kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini. Takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonesha kuwa mauzo ya bidhaa kutoka Tanzania kwenda Uganda yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 111.7 za Tanzania mwaka 2015 hadi kufikia Shilingi bilioni 631.4 bilioni kwa mwaka 2021. Wakati huo huo, thamani ya bidhaa zilizoingizwa nchini Tanzania kutoka Uganda iliongezeka kutoka Shilingi bilioni 43.8 za Tanzania mwaka 2015 hadi kufikia Shilingi 253.1 bilioni mwaka 2021.

 

Kwa upande wa gharama za usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Uganda, kuanzia mwaka mpya wa fedha ujao tarehe 1 Julai 2022, Tanzania imekubali kupunguza gharama za usafirishaji wa usafiri wa barabarani, hususani malori ya mizigo, katika barabara kuu ya kutoka Mutukula hadi Dar es Salaam kwa safari nzima kutoka dola za kimarekani 500 hadi takriban dola za kimarekani 144.

 

Pia kufunguliwa kwa njia ya usafirishaji wa mizigo kupitia Ziwa Victoria kutoka Mwanza hadi Port Bell, Kampala kutazidi kuimarisha biashara baina ya Tanzania na Uganda.

 

Ushikiriano katika Sekta ya Afya - Tanzania itaanza kununua dawa za kufubaza virusi vya ukimwi, au ARVs, kutoka Uganda ikiwa ni mojawapo ya mafanikio makubwa katika kukuza ushirikiano katika Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki. Pia wataalamu wa Tanzania watashirikiana na wale wa Uganda katika mchakato wa kutengeneza chanjo za magonjwa mbalimbali.

 

Kwa upande wa nishati - makubaliano yamefikiwa kwa kusaini Hati ya Ushirikaiano ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya kilovolt 400 kutoka Masaka nchini Uganda, hadi mkoani Mwanza.

 

Majadiliano katika sekta ya mafuta yameleta tija kwa Tanzania kutokana na wataalamu wake kupata uzoefu nchini Uganda kwa namna wanavyofanya kazi katika sekta hiyo ya mafuta.

 

Kwenye uwekezaji, Mhe. Rais Samia ameitangaza Tanzania kama sehemu salama na nzuri kwa wawekezaji kutoka Uganda kutokana na kuwa na soko kubwa, pia kuwa lango kuu la kuelekea kwenye masoko makubwa barani Afrika.

 

Majadiliano katika Sekta ya Mafuta yameleta tija kwa Tanzania kutokana wataalamu wake kupata uzoefu nchini Uganda kwa namna wanavyofanya kazi katika sekta yao ya Mafuta.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2.        ZIARA YA MAREKANI (14 - 26 APRILI, 2022)

 

WASHINGTON, D.C

 

(a)          MKUTANO WA KIHISTORIA NA MHE. KAMALA HARRIS, THE WHITE HOUSE

 

Akiwa mji mkuu wa Marekani, Washington D.C., Rais Samia alikaribishwa Ikulu ya Marekani, maarufu kama the White House, na Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala Harris, tarehe 15 Aprili 2022 na kufanya naye mazungumzo rasmi ya kiserikali. Kabla ya mkutano wao wa ndani, viongozi hao wawili walizungumza na vyombo vya habari na kusisitiza umuhimu wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani ambao umedumu kwa takribani miaka 60.

 

Katika maelezo yake, Mhe. Kamala alitaja maeneo matatu ambayo amevutiwa nayo katika uongozi wa Rais Samia, ambayo ni mageuzi ya Demokrasia, Ukuaji wa uchumi na mapambano dhidi ya Uviko-19 na changamoto nyingine kwenye sekta ya afya. Alimpongeza pia Mhe. Rais Samia kwa kuweka kipaumbele katika afya ya mama na mtoto.

 

Kwa upande wake, Rais Samia aliishukuru serikali ya Marekani kwa misaada ya maendeleo kupitia shirika lake la misaada la USAID. Alitaja baadhi ya miradi imetekelezwa na Serikali ya Marekani nchini Tanzania ambayo ina faida kubwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na PEPFAR (HIV/Aids), PMI, Feed the Future, MCC na mingineyo.

 

Kuhusu Uviko-19, Mhe. Rais alimshukuru mwenyeji wake kwa msaada wa zaidi ya dozi milioni 4.9 ambazo Serikali ya Marekani imetoa kwa Tanzania kupitia mpango wa Covax. Vilevile alishukuru kwa Tanzania kuchaguliwa kuwa moja ya nchi 11 zitakazonufaika na mpango wa Rais Joe Biden wa Global Vax.

 

KATIKA MAZUNGUMZO YAO YA NDANI, viongozi hao wawili walijadiliana ajenda zifuatazo:-

 

·      Afya;

Marekani iliahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye eneo la Uviko-19 na kuimarisha afya ya Mama na Mtoto.

 

·      Biashara na uwekezaji;

Serikali ya Marekani iko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika jitihada mbalimbali za kukuza uchumi kupitia biashara na uwekezaji. Ili kukuza biashara na uwekezaji nchini hizo mbili zilijadiliana kuhusu umuhimu wa kuwa na makubaliano ya kufungua anga ili kuruhusu ndege kutoka moja kwa moja kati ya Marekani na Tanzania kupitia mkataba wa Open Skies Agreement.

 

·      Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo;

Mhe. Kamala alimweleza Rais Samia kuwa Serikali ya Marekani iko tayari kusaidia utaalamu na ushauri kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo endapo Serikali yetu itahitaji.

·      Mabadiliko ya Kisiasa nchini Tanzania;

Mhe. Kamala alimweleza Mhe. Rais kuwa Marekani inaridhishwa na mabadiliko na kuimarishwa hali ya kisiasa yanayoendelea nchini hasa katika kipindi chake cha uongozi ambapo haki za binadamu zinazingatiwa.

 

·      Hali ya usalama katika Ukanda wa Kusini mwa Sahara;

Viongozi hao walijadiliana kuhusu hali kiusalama kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Msumbiji na namna ambavyo Tanzania imejipanga kutatua changamoto ya ugaidi katika ukanda huo. Rais Samia alimhakikishia Mhe. Kamala kuwa Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini (SADC) inafanya jitihada kusaidia kutuliza hali ya machafuko nchini Msumbiji, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizochangia vikosi vya majeshi ya SADC yanayopambana na ugaidi nchini Msumbiji. Tanzania pia imekubali kuwa mwenyeji wa kituo cha SADC cha kupambana na ugaidi ambacho tayari kinafanya shughuli zake Dar es Salaam.

Wamekubaliana kuwa Marekani iko tayari kushirikiana na SADC na EAC katika hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za ugaidi katika Ukanda huo.

 

·      Kurejeshwa kwa Tanzania katika mipango ya MCC na Feed for Future;

Katika mazungumzo yao, Rais Samia aliiomba Serikali ya Marekani kuirudisha Tanzania katika Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MCC) na mpango wa chakula wa Feed for Future. Rais Samia alimuhakikishia Mhe. Kamala kuwa serikali ya Tanzania imefanyia kazi maeneo yaliyoleta changamoto kwenye mipango hiyo mikubwa miwili.

 

 

 

(b)         MKUTANO NA WAKUU WA BENKI YA DUNIA NA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF)

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alihudhuria mkutano wa WB/IMF Spring Meeting na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Dunia, David Malpass, na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Kristalina Georgieva, ambao wote wameonesha kuridhishwa na jitihada za Rais Samia katika kipindi chake kifupi tangu ameingia madarakani na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kujenga uchumi imara, jumuishi na endelevu.

 

Katika mzunguko wa IDA-19 chini ya Benki ya Dunia, Tanzania ilitengewa kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 2.1, ambapo muda wa utekelezaji wa mzunguko huo ulifupishwa (IDA 19 frontloading) ndani ya miaka miwili badala ya mitatu ili kuziwezesha nchi wanachama kukabiliana na janga la COVID 19.

 

Hadi sasa, kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.9 zimeelekezwa katika miradi ifuatayo:

 

Project Name

Amount ($M)

Digital Tanzania Project

150.00

Land Tenure Improvement Project

150.00

Tanzania Roads to Inclusion and Socioeconomic Opportunities (RISE) Project

300.00

Boosting Inclusive Growth for Zanzibar: Integrated Development Project

150.00

Higher Education for Economic Transformation Project

425.00

Boost Primary Student Learning

500.00

Zanzibar Energy Sector Transformation and Access Project[1]

117.00

Citizen-Centric Judicial Modernization and Justice Service Delivery-Additional Financing

90.00

 

Pia Mhe. Rais Samia aliiomba Benki ya Dunia kuongeza fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bara na Zanzibar) ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ambayo maandalizi yake yamekamilika.

 

Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:

 

Project Name

Amount ($M)



Eastern Africa Regional Statistics Program-for-Results

82.00

Tanzania Transport Integration Project (TanTIP)

550.00

Tanzania Cities Transforming Infrastructure & Competitiveness (TACTIC) Project

410.00

 

Mheshimiwa Rais alisisitiza pia kuhusu Benki ya Dunia kusaidia katika programu/ miradi mahsusi wa uwezeshaji kiuchumi wanawake, vijana na wenye ulemavu pamoja na wamachinga

 

Kwa upande wa kilimo, Benki ya Dunia imeonyesha iko tayari kutoa zaidi ya  dola za Kimarekani milioni 120 kufadhili sekta ya kilimo chini ya ASDP II. Vita inayoendelea Ukraine imeleta athari katika bei za bidhaa pamoja na uhaba hususan ngano na mafuta. Hivyo, chini ya mradi wa kilimo, lengo ni kuwezesha uzalishaji mkubwa na wa kibiashara ili kutumia fursa hiyo pia kufikia soko kwa nchi Jirani.

 

(c)          MAZUNGUMZO YA MHE. SAMIA NA MKURUGENZI MKUU WA IMF:

 

Fedha za Covid-19 kiasi cha dola za Marekani milioni 567.25, sawa na shilingi trilioni 1.3; zilitumika kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu, afya na maji na kuleta ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma hizo muhimu kwa wananchi wa Tanzania. Kwa mfano, madarasa 15,000 yalijengwa kwa ajili ya shule za Sekondari (12,000) na shikizi (3,000); Ununuzi wa mashine za X-Ray na MRI ; Ununuzi wa magari ya kubebea wagonjwa; uchimbaji wa visima; na ununuzi wa magari maalum ya kuchimba visima na mabwawa; na kuimarisha sekta ya utalii.

 

Bi. Kristalina alisema amepokea maombi ya Tanzania kutaka kupewa fedha takriban dola za Marekani bilioni 1.1, sawa na shilingi trilioni 2.5 za mkopo wa masharti nafuu kupitia dirisha la ECF (Extended Credit Facility) ambapo aliahidi kwamba atayafanyia kazi ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Tanzania Bara na Zanzibar. (Kwa mud awa miaka 3).

 

Sekta zinazotarajiwa kunufaika ni pamoja na sekta za uzalishaji (Kilimo, mifugo, uvuvi); Uchumi wa Buluu; maliasili na utalii; pamoja na kukuza sekta isiyo rasmi kupitia wajasiriamali wadogo wadogo.

 

Hivyo, anaungana na mataifa mengine kusisitiza IMF kuregeza masharti ili kuzipa nchi nafasi ya kufanya mageuzi ya kiuchumi na kurejesha nchi hizo katika ukuaji wa uchumi endelevu.

 

(d)         MKUTANO NA US CHAMBER OF COMMERCE

 

Katika kikao hicho, Mhe. Rais alikuwa mgeni maalum alipata wasaa wa kusikia mitazamo, maoni na matarajio ya wawekezaji wakubwa kutoka Makampuni Makubwa nchini Marekani kwenye sekta mbalimbali za Kilimo, Viwanda, Madini, Utalii, Usafiri wa Anga, Biashara na wengineo.

 

Makubaliano baada ya kongamano ni kwamba Mwakilishi wa Chamber ya Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Kendra Gaither amekubali kutengeneza mpango wa ufuatiliaji kwa pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara chini ya Katibu Mkuu ili kuainisha mambo yatakayohitaji ufuatiliaji ndani ya kipindi cha miezi sita kuhakikisha wanapatikana wafanyabiashara na wawekezaji watakaoshirikiana na sekta binafsi ya Tanzania na Serikali katika kuongeza ushirikiano wa kiuchumi baina ya Marekani na Tanzania

Jambo ambalo limesisitizwa ni umuhimu wa kuwekeza Tanzania na manufaa ya kijiografia yanayoifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi kwa Afrika kupitia masoko ya Afrika Mashariki, SADC pamoja na njia za usafiri kupitia baharini na reli za kisasa.

 

(e)          UTIAJI SAINI – MoUs (Hati za Makubaliano)

 

Baada ya kikao hicho na wafanyabiashar, Mhe. Rais alishuhudia utiaji saini makubaliano baina ya wawekezaji mbalimbali ikiwemo na ahadi ambazo zitafungua fursa za kiuchumi.  Kwa ujumla wake makubaliano hayo yanalenga kukuza biashara baina ya Marekani na Tanzania, kuvutia uwekezaji hasa katika sekta za kilimo, nishati, viwanda na masoko. Katika makubaliano hayo kuna utiaji Saini baina ya serikali zote mbili, baina ya sekta binafsi kutoka nchi zote mbili na pia baina ya sekta binafsi na Serikali.

 

 

Makubaliano ya hati zilizosainiwa yanahushisha miradi yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 5.04 ambayo itatoa ajira 301,110

 

 

Baadhi ya Makubaliano hayo ni pamoja na:

 

Makubaliano baina ya TANTRADE (Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ambayo chini ya Wizara ya ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara) na US Chamber of Commerce ambayo ndiyo Chamber kubwa kuliko zote duniani. Makubaliano hayo:

 

§  Yanalenga kupanua wigo wa Biashara;

 

§  Kuongeza ushirikiano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani;

 

§  Kufungua fursa mpya za uwekezaji na biashara baina ya Tanzania na Marekani;

 

§  Kujenga uwezo hasa kwenye market Access na kuondoa changamoto zinazoongeza vikwazo vya biashara kupitia majadiliano na ushauri kwa serikali za pande zote.

 

Makubaliano baina ya Taifa Group ya Tanzania na kampuni kubwa ya Northern Feed Co.  ya Marekani inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta za kilimo na biashara.

Makubaliano yao yanalenga kuendeleza kilimo cha kisasa katika nafaka kwa lengo la kupunguza utegemezi na kuimarisha usalama wa chakula hasa nafaka, sukari na mafuta ya kula. 

 

Katika kuetekeza mradi huo wabia hao watawekeza kiasi cha dola za Kimarekani kati ya milioni 500 mpaka dola bilioni 1. Maeneo ambayo mradi utazingatia ni matokeo ya kulima;

 

·      Tani laki mbili za ngano;

·      Tani laki moja za sukari;

·      Tani laki moja na nusu za mafuta ya alizeti;

·      Kilimo cha Ethanol pamoja na Maharage ya Soya.

(Tani zote hizi zitazalishwa kwa mwaka mmoja).

 

Makubaliano mengine yalikuwa baina ya CTI ya Tanzania pamoja na Corporate Council on Africa (CCA) ambapo lengo ni kukuza uwekezaji katika viwanda vidogo, vikubwa na vya kati:-

 

§  Kubadilishana uzoefu na kujenga uwezo;

 

§  Kupanua fursa za ujuzi katika kubuni na kusimamia uendeshaji wa viwanda;

 

§  kutafuta fursa za pamoja baina ya pande zote zitakazoimarisha kila upande;

 

Makubaliano haya yatasaidia nchi yetu kuitumia vizuri fursa ya kuwa na viwanda vingi vidogo na vya kati ambavyo vimekuwa vikitoa ajira nyingi ili viongeze ubora wa bidhaa, ukubwa wa soko, teknolojia na ushindani kwa ajili ya soko la ndani na la nje. 

 

Makubaliano mengine yalikuwa ni kwenye mikataba miwili ya uwekezaji kwa kampuni za Daya Group Investment Limited (Kampuni ya Marekani na Hong Kong) na Kampuni ya Wabi International Limited. (Wamarekani)

Pamoja zina mpango wa kuendeleza uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii. Mkataba huu ulisainiwa baina ya wawekezaji binafsi wa Daya Investment pamoja na Wabi International Limited kama makampuni ya uwekezaji pamoja na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kwa lengo la kuwasaidia wawekezaji kupatiwa taarifa na kuwezwesha kukamilisha taratibu zao.

 

Kwa ukanda wa Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Mara, lengo ni kuongeza biashara ya utalii kwa kuweka miundombinu ya kisasa ikiwemo mahoteli na uwekezaji katika shughuli mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani.

 

Kwa pamoja makampuni haya mawili yana mpango wa kuwekeza dola za kimarekani milioni 350. Miradi hii inashirikiana na wataalamu maarufu duniani walioko Marekani kwenye uwekezaji wa utalii. Makampuni hayo ni Howard Backen Chateau Designer, Toam Doack, Golf Course Designers pamoja na Master of Wine Bill Harlan

 

Makubaliano mengine ni baina ya wawekezaji wa Marekani kupitia FE Jordan and Associates wakishirikiana na wawekezaji wa ndani wakiwakilishwa na kampuni ya SJS pamoja na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara katika kuendeleza kanda maalum ya kiuchumi kwenye mikoa ya kusini kupitia Bandari ya Kilwa.

 

Makubaliano yaliyopitiwa ni kwa wizara kuratibu maandalizi na mazungumzo yao na Mamlaka ya Bandari, Shirika la Reli pamoja na taarifa za upembuzi yakinifu wa mradi. Lengo ni kufungua fursa za kiuchumi kwa kuweka ukanda maalum kwaajili ya usafiri na lojistiki, kuimarisha bandari na maendeleo ya eneo la viwanda.

 

Makubaliano mengine ni baina ya Tanzania Commodity Exchange pamoja na kampuni kubwa ya  STONEX ambayo ni kubwa duniani katika masoko ya bidhaa ikiwemo kilimo.

Lengo la makubaliano haya ni kuongeza uwezo wa Tanzania Commodity Exchange kutafuta masoko ya bidhaa na kukuza biashara kwa kutafuta bei nzuri katika masoko ya dunia.

Kwa STONEX wanazungumzia kutafuta soko la bidhaa lenye thamani ya dola bilioni 1 kwa kuanzia ikimaanisha kuwa bidhaa zote zitakazotafutiwa soko zitakuwa na thamani ya dola bilioni 1

 

Pamoja na utiaji saini makampuni mengine yalipata fursa ya KUTANGAZWA kwamba yapo katika hatua mbalimbali za mchakato wa ushirikiano na taasisi na makampuni ya Tanzania.

Makampuni hayo ni pamoja na; Upepo Energy (YA Marekani na ya Binafsi) ambayo ipo katika mazungumzo na TANESCO kwaajili ya mradi wa kuzalisha Megawatt 100 za umeme wa upepo pamoja na megwatt 45 kwa ajili ya umeme wa jua.

 

Kampuni nyingine ni Astra Energy (YA Marekani na ya Binafsi) ambayo ina lengo la kuwekeza dola za Kimarekani milioni 180.

 

Pia Mheshimiwa Rais alipata fursa ya kusikia utayari wa kampuni ya Parallel Wireless ambayo inalenga kusambaza vifaa 99 vya minara ya mawasiliano na itashirikiana na TTCL.

 

Kampuni ya mwisho iliyotambulisha nia yake ya ushirikiano ni kampuni ya Crane Currency. Kampuni hii yenye uzoefu wa miaka mingi katika masuala ya fedha inalenga kushirikiana na Benki kuu katika utambuzi wa noti bandia, kuimarisha ubora wa noti zetu na kujenga uwezo wa benki kuu katika kutambua uharamia wa kifedha. 

 

 

ZIARA YA DALLAS, TEXAS:

 

Katika ziara ya Mhe. Rais nchini Marekani, alialikwa kutembelea jiji la Dallas, Texas ambapo Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dr. Ashatu Kijaji alimuwakilisha. Ziara hiyo iliambatana na kongamano kubwa baina ya wafanyabiashara wa Tanzania, viongozi wa serikali na Balozi Dkt. Kanza anayeiwakilisha Tanzania katika nchi za Marekani na Mexico.

 

Katika ziara hiyo Meya wa jiji la Dallas Eric Johnson alionesha kufurahishwa na hatua nyingi ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, amefikia katika kukuza Diplomasia ya kiuchumi, kuitangaza Tanzania na kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani. Meya aliwahakikishia washiriki kuwa jiji la Dallas lina mkakati pekee wa kushirikiana na Tanzania katika kukuza uchumi, biashara na uwekezaji.

 

Katika ziara hiyo Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara iliingia makubaliano na Meya wa jiji la Dallas katika kukuza ushirikiano baina ya jiji hilo na Tanzania hususan katika maeneo yafuatayo;

·      Kusimamia ukamilishaji wa makubaliano ya “Open Skies Agreement” ambapo kutakuwa na uwezekano wa kuwa na ndege za moja kwa moja kutoka Dallas Mpaka Tanzania. Lengo ni kukuza utalii kwa kuwa na ndege za kubeba watalii kutoka Dallas, kukuza biashara hasa ya mboga na matunda na kwa kuanzia wako tayari kununua maparachichi.

 

·      Kuongeza muinguliano baina ya Tanzania na Marekani kwa kuwezesha abiria wengi kuweza kufika Dallas na mwisho kuifanya Tanzania kama kitovu cha kuiunganisha Dallas na Afrika.  Mpango huu utakuwa na manufaa makubwa kwa kupunguza gharama za usafirishaji pamoja na muda wa kusafiri baina ya Afrika na Dallas. Kwa mujibu wa Meya uwanja wa Dallas Fortworth ni kati ya viwanja ambavyo vina ndege nyingi na abiria wengine Duniani. Ni uwanja wa ndege wa tatu Duniani unaopokea abiria wengi.  Third busiest Airport in the World.

 

·      Makubaliano mengine ni kuwa na mkakati wa pamoja wa kuvutia wawekezaji, kupanua biashara na ushirikiano kwa faida ya uchumi wa pande zote mbili.

 

·      Aidha Meya huyo aliahidi kufanya ziara nchini Tanzania. Mpango wa utekelezaji wa makubaliano hayo uwe umekamilika katika kipindi cha miezi 6.

 

ZIARA YA WISCONSIN:

 

Tarehe 19 Aprili 2022, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, alifanya ziara katika Kampuni ya SC Johnson iliyopo Wisconsin, Marekani, akiongozana na Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, pamoja na maafisa waandamizi serikalini. Kampuni ya SC Johnson inajishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za usafi wa majumbani na kemikali za kudhibiti wadudu wanaodhuru na waenezao magonjwa, ikiwemo Malaria, Dengue, Zika na Chikungunya.

 

Katika ziara hiyo, Mhe Rais alifanya mazungumzo na mwenyeji wa kampuni hiyo, Dkt. Hubert Fisk Johnson, ambaye ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya SC Johnson.

 

Mtendaji wa SC Johnson, Dkt Fisk amekubali kusaini Hati ya Makubaliano itakayowezesha ujenzi wa Zahanati kwenye Halmashauri zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

 

Mtendaji huyo ameahidi kusaidia kuimarisha miundombinu katika chuo cha udhibiti wa wadudu wanaodhuru na waenezao magonjwa kilichopo Muheza, Mkoani Tanga (Muheza Vector Control Training Centre) – (Kinafundisha wataalam) kwa kushirikiana na Taasisi za Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (National Institute for Medical Research) pamoja na Taasisi ya Afya ya Ifakara (Ifakara Health Institute).

 

PLASTIKI

Katika ziara hiyo kwenye kampuni ya SC Johnson. Tanzania ilipata fursa ya kujifunza jinsi Kampuni hiyo imeweza kuzisaidia nchi za Indonesia na Brazil katika kudhibiti taka zitokanazo na plastiki. Vilevile, wamekubali kuisaidia Tanzania katika jitihada za udhibiti wa taka zitokanazo na bidhaa za plastiki. Kupitia uwekezaji wa Kampuni hii, Tanzania inatarajia kupata msaada usiopungua shilingi za kitanzania bilioni 80 katika kufadhili miradi hiyo.

 

ROYAL TOUR

Swali la 1:

Ni nini Royal Tour?

 

Ø Ni makala maalum inayohusisha Wakuu wa Nchi waliopo madarakani ili kuzieleza nchi zao na kuzitangaza kimataifa katika sekta mbalimbali. 

 

Ø Tanzania ni nchi ya 9 kushiriki program hii ambayo pia humpa nafasi kiongozi husika kuzindua Makala hayo nchini Marekani, kupata nafasi ya mahojiano na vyombo vikubwa vya habari na kukutana na wadau mbalimbali wa biashara, utalii na uwekezaji ana kwa ana ili kuwavutia kuja nchini kuwekeza. Nchi nyingine zilizoshiriki Royal Tour ni:-  Jordan, New Zealand, Poland, Mexico, Ecuado, Peru, Israel, Rwanda na sasa Tanzania.

Ø Sababu nyingine ya kutumia Marais walio madarakani ni kujenga Imani kwa watazamaji yaani watalii na wawkezaji.

 

Swali la 2:

Nani kadhamini Filamu hii?

Ø Sehemu kubwa ya filamu hii imetokana na michango ya sekta binafsi hasa utalii, biashara, viwanda na sekta ya huduma.

 

Swali la 3:

Faida zipi zimepatikana/zitapatikana?

Ø Kwanza, filamu hii imeitangaza nchini na inaendelea kufanya hivyo kwa miaka mingi kwani imewekwa pia katika mitandao mikubwa duniani kama Amazon na Apple Tv na itaoneshwa katika channeli 350 nchini Marekani zinazowafikia wamarekani zaidi ya milioni 200.

Pili, Rais akiwa Marekani amekutana na wawekezaji wakubwa katika sekta za utalii, biashara na filamu—hivyo katika siku zijazo Taifa linatarajia kupokea wawekezaji na watalii wengi. 

Filamu ya Tanzania The Royal Tour imebainisha kuwa Mlima Mrefu kuliko yote Barani Afrika (Mlima Kilamanjaro upo Tanzania) na sio nchi nyingine.

 

Madini ya Tanzanite: Filamu ya Tanzania The Royal Tour imeelezea kwa kina kuwa Madini haya ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu na sio nchi nyingine.

 

Utunzaji wa Misitu: Kipande kidogo kilichoonesha baadhi ya misitukule Ngorongoro kimewavutia Shirika la Carbon Credit na kuahidi kutoa Fedha kwa ajili ya uhifadhi wa misitu.

 

Wataliii mbalimbali wameahidikuja nchini mara baada ya kuona Filamu hiyo ya Tanzania The Royal Tour

 

Swali la 4:

Baada ya premier ndio mwisho wa kutangaza Nchi?

 

Ø  Katika kuhakikisha Tanzania yenye raslimali nyingi inaendelea kutangazwa kimkakati Mhe Rais aliunda Kamati Maalum ya Kuitangaza Tanzania na kazi ya kubuni miradi mbalimbali ya kuitangaza nchi kama ilivyofanyika kwa Royal Tour na itaendelea.

Ø  Aidha, makala nyingine za filamu ya Royal Tour zitatolewa katika siku zijazo ikiwa ni sehemu ya pili na ya tatu.

§  Mengine mengi yalofanyika

§  Kukutana na Diaspora

§  Kukutana na Wafanyabiashara wakubwa

§  Tasnia ya filamu

§  Paramount Studios

No comments:

Post a Comment

Pages