May 19, 2022

VETA YABUNI KIFAA CHA KUFUNDISHIA MASUALA YA ANGA


Mbunifu wa kifaa cha kufundishia Mfumo wa Jua na Sayansi ya Anga Ernest Maranya akielezea kuhusu kifaa hicho kinavyofanya kazi.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),imebuni kifaa cha kufundishia Mfumo wa Jua na Sayansi ya Anga  wenye lengo la kurahisisha mchakato wa kufundishia katika shule za msingi na sekondari ili kuwasaidia watoto katika kusoma kiuhalisia ambacho tayari kimepewa kibali cha kutoa elimu katika Mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza Mei 18, 2022 katika maonyesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia( MAKISATU), kwa mwaka 2022 ambayo yameendaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP),kupitia mradi wake wa FUNGUO, yanayofanyika katika viwanja vya Jamuhuri jijini hapa.

Mbunifu kutoka VETA  ambaye anatambulika katka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), na Mamlaka ya Anga Ernest Maranya  amesema kuwa ubunifu huo tayari umeshafanyiwa tathimini na  Taasisi ya Elimu Tanzania kwa lengo la kurahisisha kifaa hicho kitumike kama nyenzo ya kufundishia katika mitaala kwa shule za msingi na sekondari na baade vyuo vikuu ili kupata misingi ya kufundishia  wanafunzi hao watambue namna kinavyofanya kazi angani.

Amesema kuwa kwa bahati mbaya elimu hiyo hapa nchini kwa muda mrefu wanafunzi walikuwa wakifundikwa kwa Nadharia ambayo haina vifaa wezeshi hivyo kifaa hicho kina muwezesha mwanafunzi huyo katika kuona uhalisia namna ya jua, sayari na vimondo  ambavyo vinavutana angani.

" Lengo la elimu hii ni kujenga msingi wa kuvirisisha vizazi kufanya maandalizi ya hapo baadae ili taifa lije kuwa na wataalamu watakaokuwa na uthubutu wa kufanya utafiti wa mambo ya anga badala ya kusubiri taarifa za utafiti unaohusiana na mambo ya anga kutoka nchi mbalimbali," amesema Mbunifu huyo.

Ameongeza kuwa mataifa mengine yanapofanya utafiti kuhusu mambo ya anga kuna vitu vya siri wanavyogundua na yanakuwa ni siri zao ambapo hawaruhusu nchi nyingine kujua.

Mbinifu huyo Maranya amesema kuwa tayari kifaa hicho kimetambulika na mamlaka husika kilichobaki ni kuboresha baadhi ya marekebisho kwa mujibu wa mamlaka hizo

No comments:

Post a Comment

Pages