June 17, 2022

GPE kuipatia Tanzania msaada wa Bilioni 269.1 kwa ajili ya sekta ya elimu

 

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof. Eliamani Sedoyeka, akitoa hotuba yake wakati akifungua rasmi warsha ya wadau wa elimu jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika warsha hiyo.

 Mbunge wa Ubungo ambaye pia ni mshauri na mtaalum wa elimu, Kitila Mkumbo, akichangia mada katika warsha hiyo..


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof. Eliamani Sedoyeka (kulia), akifuatilia mada katika mkutano huo.

 

SERIKALI inatarajia kupata msaada wa dola za Marekani shilingi milioni 117 sawa na shilingi bilioni 269.1 za Tanzania kutoka Ushirika wa Kimataifa wa Kusaidia Maendeleo ya Elimu Duniani (GPE).
 
Fedha hizo  kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu ya Msingi na Sekondari nchini.
 
Akizungumza katika Warsha ya elimu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022.
 
Mbunge wa Ubungo ambaye pia ni mshauri na mtaalum wa elimu, Kitila Mkumbo amesema Dola milioni 117 zinazotolewa na GPE zitasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza, kuwajengea uzoefu walimu, kuwapa motisha, pia uboreshaji wa menejimenti na uongozi wa shule.
 
Amesema maeneo hayo yanamepewa kipaumbele kwa kuzingatia hali halisi ya mahitaji ya elimu kwa sasa.
 
"Serikali imekuwa ikiwekeza fedha katika mambo mbalimbali yaliyopo katika sekta ya elimu hivyo uchaguzi wa vipaumbele umezingatia maeneo ambayo bado yanaonekana na mapengo ili kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu.”Amesema Kitila.
 
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Eliamani Sedoyeka amesema GPE imekuwa msaada kwa mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania ambayo ilijiunga rasmi 2013 na mwaka 2014 ilipata msaada wa dola milioni 94.8.
 
Amesema fedha hizo zilitumika katika programu ya miaka minne iliyolenga kuongeza ujuzi kwa wanafunzi katika stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
 
Amesema fedha zinazoombwa sasa ni awamu ya tatu zikilenga kuboresha maeneo mbalimbali katika sekta ya elimu ikiwemo  kuangalia mabadiliko ya kimfumo pamoja na kutengeneza sera ambazo zitapelekea maboresho katika mfumo wa elimu nchini.
 
Aliongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani alisitiza juu ya kuwajengea uwezo wahitimu katika ngazi mbalimbali kuwa na ujuzi wa uzalishajimali utakaowawezesha kuweza kujiajiri na kuajiri wengine.
 
“Ili kuyatimiza hayo serikali imejipanga katika kuhakikisha inawekeza katika kuboresha mifumo, sera na miundombinu katika sekta ya elimu.”Amesema.
 
Nae, mwakilishi kutoka GPE Lusinda Ramos amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha elimu nchini.
 
“Tumekuwa tukitoa fedha kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa elimu tangu Tanzania kujiunga na GPE mwaka 2014 na tutaendelea kufanya hivyo katika uboreshaji,” – Lusinda Ramos mwakilishi GPE.
 
Pia ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua katika Sekta ya elimu ambayo matokeo yake yanaongezeka kila mwaka.
 
Kwa upande wa rais wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu,  (TAPIE), Mahmoud Mringo, amesema jambo linalofanyika ni jema kwa kuwa serikali inatafuta rasilimali  ambazo hatuna ili tuweze kujenga uwezo sahihi wa kuweza kuwapeleka watanzania katika elimu iliyobora zaidi  na hasa elimu ambayo itamuwezesha mwanafunzi anapohitimu  shule aweze kujisimamia mwenyewe katika maisha yake ya kila siku.

 

No comments:

Post a Comment

Pages