June 16, 2022

Madawati ya Jinsia na Watoto toka mikoa yote Tanzania watoa elimu ya ukatili wa Kijinsia Arusha

 


 Na Gasto Kwirini wa Jeshi la Polisi Arusha

Mkuu wa Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP Maria Nzuki leo tarehe 15.06.2022 ameongoza Maofisa, Wakaguzi na Askari toka madawati ya jinsia na watoto Mikoa yote ya Tanzania kwa ajili ya kutoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Arusha.

DCP Nzuki amesema kuelekea siku ya mtoto wa Afrika  inayofanyika kitaifa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara tarehe 16.06.2022 amesema wakiwa mkoani Arusha watatoa elimu katika kata zote za Jiji la Arusha ikiwemo shule za msingi.

Sambamba na hilo amesema anaimani kuwa jamii itabadilika baada ya kupata elimu ya hiyo kwani vitendo hivyo havikubaliki katika jamii na vinaadhibiwa kisheria.

Aidha ametoa wito kwa Wananchi kubadilika ambapo amewataka kuwatunza watoto wao na kukemea baadhi ya wazazi kuwaacha watoto wao bila ya uangalizi ama kulelewa na wasichana wa kazi hali ambayo inapelekea vitendo vya ukatili kuongezeka katika jamii.

Bwana Mpeli Ally kalonge toka *SOS Children's Villages* ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali amesema ukatili dhidi ya watoto unadumaza haki zao na kuwa na madhara makubwa kwa maendeleo yao ambapo amesema wao kama shirika wanaowajibu wa malezi ya watoto pamoja uimarishaji wa familia kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na usalama wa mtoto.

Kwa upande wa Wananchi wa jiji la Arusha wamefurahishwa na elimu iliyotolewa ambapo wamesema imewasaidia kujua kuwa watoto wote wana haki sawa katika kupewa huduma mbalimbali.

Zaidi ya Askari 90 wa vyeo mbalimbali ambao waligawanywa katika kata zote za Jiji la Arusha walipata fursa ya kutoa elimu za ukatili katika mashule na maeneo ya mikusanyiko.

No comments:

Post a Comment

Pages