June 09, 2022

RAIS SAMIA AANGIZA VIONGOZI KUSIMAMIA MIRADI YA MENDELEO KWA MALENGO KUSUDIWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi katika mji mdogo wa BiharamuloZ

Sehemu ya wananchi waliompokea wakisikiliza hotuba yake
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi wilayani Biharamulo ikiwa ni katika ziara ya siku 3 Mkoani Kagera.

Rais Samia amesema kuwa fedha nyingi zimekusanywa  na zitaendelea kuletwa kwa wananchi hivyo hakuna haja ya kukaa nazo au kuona zinatuna kwenye mifuko bure hivyo ni vyema viongozi walioaminiwa wasimamie  vyema miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na serikali kwa malengo husika.

" Kwa maneno ya mkuu wa Mkoa ,wakuu wa wilaya na wabunge simamieni vyema fedha hizo kwa matumizi lengwa"alisema Rais Samia.

Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja  Jenerali Charles amempongeza Rais Samia kwa namna anavyowajali wananchi katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages