June 01, 2022

Rais Samia ahudhuria Tamasha la Dream Concert na Kuzindua Kitabu cha Msanii wa Hiphop Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Serena Jijini Dar es Salaam

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Serena pamoja na Msanii wa Muziki wa Hiphop nchini Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wasanii wa muziki wa Hiphop na Bongo flava katika maadhimisho ya miaka 30 ya Msanii Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ya kuwa katika fani hiyo kwenye Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Sasha Joseph Mbilinyi mtoto wa Msanii wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabu cha Msanii Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpa Tuzo Msanii wa Muziki wa Hiphop nchini Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ya kuthamini mchango wake katika Sanaa na kuzalisha ajira kabla ya kuzindua kitabu cha msanii huyo chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa Muziki wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mara baada ya kuwasili Serena kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la maadhimisho ya miaka 30 ya msanii huyo.


No comments:

Post a Comment

Pages