June 10, 2022

RAS SENEDA AFUNGUA MAFUNZO YA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII MAFINGA


Katibu Tawala Mkoa wa Iringa  Happiness Seneda akiongea na watumishi ambao walikuwa wanapata mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii. Baadhi ya viongozi wanaosimamia mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii.

 

Na Fredy Mgunda, Iringa

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa  Happiness Seneda amefungua mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii  wa Halmashauri ya Mji Mafinga.

Alisema mfumo utaanza rasmi kutumika tarehe 1/7/2022 ambapo utarahisisha vikundi vyote kuingizwa kwenye mfumo huo, usimamizi wa marejesho, utoaji w mikopo utakuwa wa haki na hakuna mtu atakopa kwenye vikundi viwili kwa kufanya udanganyifu kwani mfumo utamkataa.

Seneda ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuona wananchi wanaondokana na umaskini na wanaweza kusimamia uchumi wao, hivyo anatarajia mafunzo hayo  yalete matokeo chanya na kuondokana na changamoto zilizokuwepo hapo nyuma katika ukopeshwaji, urejeshaji na usimamizi wa mikopo hiyo ya makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu.

Aidha Kuhusu zoezi la Kitaifa la SENSA ya watu na makazi, Katibu Tawala amesema Elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili waweze kushiriki zoezi hilo kikamilifu tarehe 23 Agosti kwani litasaidia kupanga mipango ya Serikali kwa sekta zote.

Mafunzo hayo, yametolewa na wawezeshaji ngazi ya mkoa wa Iringa na kuhudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Idara  pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu, Charles Tuyi Afisa Mazingira

 

No comments:

Post a Comment

Pages