June 13, 2022

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA KUWAFANYIA USAILI WAOMBAJI 700


Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakam, Profesa Elisante  Ole Gabriel. 

 

MWANDISHI WETU

TUME ya Utumishi wa Mahakama imewaita kwenye usaili waombaji 700 waliotuma maombi ya kazi katika kada tisa kati ya 15,484 huku idadi ya wanawake ikiwa kubwa kuliko wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumapili, Juni 12,2022 Katibu wa tume hiyo, Profesa Elisante  Ole Gabriel amesema, watanzania 15,484 wametuma maombi ya kazi zilizotangazwa ikiwamo, Hakimu Mkazi Daraja la pili, Katibu Mahsusi, Afisa Hesabu na Afisa Hesabu Msaidizi.

Nyingine ni, Udereva, Afisa Utawala, Afisa Utumishi na ,mMtunza Kumbukumbu Daraja la pili.


Alisema usaili huo utafanyika Juni 15, 2022 na kwamba tume imetenga vituo   sita tofaut.

Alitaja vituo hivyo kuwa vitakuwa katika  Kanda ya Mahakama ambazo ni, Dar es Salaam, Morogoro, Mbeya, Dodoma, Mwanza na Arusha.

"Waombaji wote wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usaili wa maandishi Juni 15,mwaka huu kwenye vituo nilivyovitaja na majina yataorodheshwa kwenye tuvuti ya tume isipokuwa mahakimu watafanyia usaili wao Dar es Salaam kutokana na sababu maalum" Alisema Profesa.

Alisema watanzania wasikubali kutapeliwa kwamba watoe fedha ili wasaidiwe kupata kazi, mfumo wa tehama umefanya kazi hiyo na mpaka tumefanikiwa kupata watu 700 kati ya elfu 15 walituma maombi hayo.

"Mfumo wa Tehama tunaotumia hakuna kubebana wote watakuja na kufanya usaili wao kwa njia digitali na si kuandika kwa mkono, watanzania wengi wanaipenda Mahakama maombi hayo yote ni ya vijana ambao hawajawahi kiajiriwa"Alisema Profesa Gabriel.

Aidha, alisema kuwa Mahakama inazingatia 50/50 kwa kuwa kada ya udereva idadi ya wanawake ni, 18 na wanaume ni, 1972, nafasi zilizotangazwa ni, 35 na walioitwa kwenye usaili 110 ambapo alisisitiza kutoa kipaumbele kwa wanawake.
 

No comments:

Post a Comment

Pages