June 14, 2022

WAZIRI BASHE: ATAKAE SAFIRISHA MAZAO BILA KIBALI MALI ZAKE ZITATAIFISHWA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amewataka wafanyabishara  wa Mazao wanaosafirisha nje ya nchi  kuomba kibali,  leseni ya usafirishaji kabla hawajaanza safari ili kuepuka msongamano wa malori mipakani ambapo ndipo wanapoenda kuomba leseni hiyo.

Pia amesema kuwa kama serikali wakimkamata mfanyabisha anayevuka mipaka bila kibali cha usafirishaji wanamkamana na kutaifisha  mali zake pamoja na kumchukulia hatua za kisheria.

Waziri Bashe ameyasema hayo  jijini Dodoma Juni13,2022, wakati akizungumza na waandishi  wa habari kuhusu ukiukwaji wa utarabu wa kuomba leseni hiyo amesema kuna zaidi ya malori 40 yapo katika mpaka wa Namanga  mengi hayana leseni ya usafirishaji huku akisisitiza  utarabu wa kupata leseni upo mtandaoni na hakuna gharama na  sio kuanza safari na kwenda kusababisha foleni mipakani mwa nchi.

Amesema wanafanya utarabu wa kuwasaidia wafanyabishara hao ili waweze kusafirisha mazao hayo na kwamba hawazui watu kufanyabiashara hiyo nje ya nchi hivyo wanatakiwa kukata leseni wawe nayo mkononi kabla ya kuanza safari.

" Kumeibuka tabia ya mtu anaenda kununua mazao kijijini halafu hajaomba leseni ya kusafirishia mazao yake ambayo inaombwa kupitia mtandaoni, mtu huyu anaondoka na Lori lake moja kwa moja hadi mpakani akifika huko ndo anaanza kuomba leseni. Hii ni kinyume na utarabu lazima tufanye biashara kwa utarabu kama nchi tunapotoa vibali  vya kusafirishia Siri yake ni kujulikana mazao haya yanatoka nchi gani," amesema Bashe.

Waziri Bashe ameongeza kuwa kama nchi hawawezi kufunga mipaka ya usafirishaji wa mazao wanawaruhusu watu kufanyabiashara kuuza na kununua hivyo hawazui biashara hiyo kwa sababu kitendo cha kufunga mipaka maana yake wanaondoa biashara yote  na atakayepata hasara ni mkulima.

No comments:

Post a Comment

Pages