July 17, 2022

ACT WAZALENDO YAHASISHA ZOEZI LA SENSA


 
Na Mauwa Mohammed Zanzibar


Mwenyekiti wa chama Cha ACT Wazalendo  Mhe. Juma Duni Haji amesema moja katika masuala yanayoleta matatizo makubwa katika visiwa vya Unguja ni umiliki wa ardhi na makaazi.

Hayo aliyasema  mbele ya timu ya uhamasishaji wa zoezi la Sensa  pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa ACT Wazalendo  wa mkoa wa kaskazini A  Unguja  katik kijiji cha Shangani.

Duni alisema umiliki wa ardhi na  ongezeko la watu visiwani ni jambo ambalo linahitaji kuangaliwa kwa makingi na kulipatia ufumbuzi wakudumu.

Hata hivyo alisema zoezi la sensa yawatu na makaazi linaweza kuleta ufumbuzi wa kudumu.

Aidha alitaka wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ili kurahisisha mipango ya maendeleo ambayo itamnufaisha kila mwananchi.

Mapema katika kikao hicho kaimu Naibu katibu mkuu wa ACT Wazalendo Salim Abdalla Bimani ameiomba  tume hiyo kushirikisha vijana wa vyama vyote katika kazi ya i kuhesabu watu badala kuwemo watendaji  wa chama kimoja..

Alisema miaka kumi iliyopita hapakuwa na mashirikino ya masuala ya sensa kwani yalionekana kama ni zoezi la siasa ya upande mmoja.

Alisema Mara hii kunaonekana kutakuwa na mashirikiano makubwa ya kufanikisha zoezi hilo.

Hivyo alisema ni vyema zoezi hilo kushirikisha vyama vyote vya siasa badala ya hivi sasa kuonekana kuwepo sura ya watendaji wa upande mmoja 

"ACT tunahitaji kushirikishwa mana bado wanaoshughulikia sensa kuna sura ya chama kimoja ili tufanikiwe kwenye Sensa hii tunahitaji tushirikishwe" alisema Bimani.

Aidha alisema vijana wao ndio wanaotambua watu katika shehia zao kushirishwa kwao kutasaidia kurahisisha zoezi hilo.


Kwa upande wake afisa mahusiano ofisi ya mtakwimu mkuu bi Safia Abdalla Ali alisema serikali imekabiliwa na shughuli kubwa kuhesabu watu yenye lengoo la kupata takwim sahihi zitazoiwezesha serikali na wadau wengine kupanga mipango kwa usahihi.

Alisema zoezi hilo litakuwa ni la nchi nzima kwa sasa wapo katika zoezi la uhamasishaji na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa sensa.

Pia alisema sensa ya watu na makaazi ni moja zoezi muhimu linalokusanya taarifa za kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia siku ya sensa.

Tanzania itafanya sensa ya watu na maazi mwezi Agosti 23 mwaka huu ikiwa ni mara ya sita kufanyika ambapo mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1967,1978, 1988, 2002, 2012 na hivi sasa 2022.

No comments:

Post a Comment

Pages