Mbunifu Zacharia Lymo akionyesha mfumo unavyofanya kazi.
Na Asha Mwakyonde
CHUO Cha Kumbukumbu Mwalimu Nyerere kimekuja na bunifu ya kuwasha Bomba 'Pumb' kwa mfumo wa kutumia simu ya mkononi kujaza maji na kupandisha juu ya kwenye tenki.
Akizungumza Julai 7, 2022 katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mwanafunzi na Mbunifu wa mfumo huo Zacharia Lymo amesema mtu anapojaza maji kwa kutumia simu yake kwenye tenki likishajaa unajizima katika ujazo unatokiwa bila kumwaga maji.
Lymo amefafanua kuwa lengo la kubuni mfumo huo ni kutatua changamoto zinazotekea majumbani au viwandani ikiwa ni pamoja na kupunguza upotevu wa maji pindi yanapomwagika wakati wa kujaza kwenye tenki kukiwa hakuna uangalizi.
" Mfumo huu umechukua muda wa miezi 3 hadi kufikiria na kuutengeneza hadi kufikia hapa gharama yake ni laki 500,000," amesema.
Ameongeza kuwa kwa sasa Mbunifu huyo yupo katika mchakato wa kusajili kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), na kwa sasa mfumo huo upo chini ya uangalizi wa Chuo hicho.
No comments:
Post a Comment