July 19, 2022

NIT yawataka wanafunzi kuchangamkia fursa katika miradi ya kimkakati

Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Juma Manday, kifafanua jambo kwa watu mbalimbali waliojitokeza katika banda lao kuangalia fursa zilizopo katika masomo maalumu yanayoendana na miradi ya kimkakati.

Afisa Udahili Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Ally  Mahamood, akiwapa maelekezo ya namna ya kujiunga na chuo hicho baadhi ya wanafunzi waliojitokeza katika banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


CHUO  cha Taifa Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kimewataka wahitimu wa kidato cha sita na wananchi wengine wenye nia ya kufanya kazi katika miradi ya mbalimbali ya kimkakati inayoendelea kujengwa nchini  kujiunga na chuo hicho Ili kujiweka vizuri kuipata fursa hiyo.

Akizungumza wakati wa maonyesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, Mhadhiri wa Chuo Juma Manday amesema ili kuhakikisha miradi inapata wataalam wa kutosha, NIT iliamua kuanzisha masomo maalumu yanayoendana na miradi hiyo.

Alitolea mfano wa miradi  ambayo chuo hicho kimenzisha masomo yake kuwa ni pamoja na mradi wa Reli ya Kisasa 'SGR' ,Ujenzi wa miradi ya gesi, Usafiri wa anga pamoja na usafiri wa majini.

Manday amesema katika kutimiza azma hiyo chuo hicho kimeanzisha masomo ya Shahada ya uhandisi katika fani ya mafuta na gesi, shahada ya Uhandisi katika utengenezaji wa ndege, usanifu na utengenezaji wa Meli , pamoja na shahada katika usafirishaji wa Barabara na Reli.

" Chuo chetu ni cha kimkakati kama mnavyofahamu, masomo mengi ambayo yanafundishwa yanashahabiana vizuri na miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali, lengo kuzalisha wahitimu wengi ambao watakuja kufanya kazi katika miradi hiyo" amesema Manday

Aidha amesema mbali na fani hizo pia NIT inafundisha masomo katika fani mbalimbali zikiwemo za uhudumu wa ndani ya, uhandisi wa magari, udereva na fani zinginezo ambazo msingi wake ni kumuandaa muhitimu kuingia katika soko la ajira.

Maonyesho hayo ya 17 yanayohusisha vyuo mbalimbali zaidi ya 75 lengo lake ni kuwawezesha wanafunzi kupata fursa ya kuomba nafasi ya kudahiliwa katika vyuo mbalimbali vya ndani na vya nje kwa mwaka wa masomo 2022/2023.

No comments:

Post a Comment

Pages