July 14, 2022

SIMON MSUVA ATEMA NYONGO

Mchezaji wa Kimataifa Simon Msuva amezungumza na Waandishi wa habari leo baada ya FIFA kuagiza Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa Mchezaji huyo zaidi ya dola za kimarekani laki 7 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 1.6 baada ya kushinda kesi ya madai aliyoifungua kuhusu malimbikizo ya mishahara na ada ya usajili.

Simon Msuva amefunguka mambo mengi ikiwemo mambo aliyokuwa anafanyiwa na klabu yake ya zamani Wydad Casablanca amesema "Nimepata matatizo Morocco kuhusu mambo ya mikataba na dada yangu ameshagusia, kwa upande wa wachezaji wenzangu ambao wanahitaji kufika malengo ambayo nimefikia mimi, wanapaswa kuwa na usimamizi mzuri".

"Simon wa miezi saba ameshapita sasa anaanza upya, tuangalie sasa Simon atakuwa wapi, maana ameshashinda kesi, nitaweka wazi hilo sio kwa sasa kama nitacheza ndani au nje ya Tanzania”

“Kwa sasa tunashukuru kwa kushinda kesi sio nguvu zetu ni nguvu za Mungu, nimepitia magumu sana nilikuwa sitaki hata Timu ya Taifa niitwe lakini Viongozi wamenitengeneza kiakili na nimeweza kuperfom kwa uwezo niliokuwa kusaidia nchi yangu japo sio kwa uwezo mkubwa sana kama ambavyo watu walivyonizoea".

No comments:

Post a Comment

Pages