July 18, 2022

SUZA chawakaribisha wanafunzi kujiunga na kozi mpya za masomo mwaka 2022/23


Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar Khadija Sadiq Mahumba, akitoa maelekezo Kwa baadhi ya Wanafunzi waliotembelea Banda la SUZA la TCU.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

 

Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) kinaendelea kuunga mkono sekta ya elimu nchini Kwa kuanzisha kozi mpya  ikiwemo ya  Shahada ya Uzamivu kwenye Sayansi ya Teknolojia ya Habari (IT) katika mwaka wa Masomo 2022/ 2023.

 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko wa SUZA Khadija Sadiq Mahumba wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). 

 

Amesema kuwa chuo hicho kinatarajia kudahili wanafunzi wapatao 2000 Kwa programu mbalimbali zikiwemo za Elimu,Afya,Kilimo kwa ngazi mbalimbali ikiwemo  Cheti, Astashahada Shahada, Shahada ya Uzamili na Uzamivu.

 

Amesema kuwa kwa mwaka huu wa masomo chuo hicho pia kinatarajia kutoa programu ya Shahada ya Uzamivu( Phd) ya Lugha ya kiswahili ,na kwamba amewaomba wanafunzi wanaotaka kujiunga na SUZA wachangamkie fursa hizo.

 

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Uhusiano na Masoko SUZA ,amesema kwamba Chuo hicho kinatoa programu za Kozi za Utalii ambapo wanafunzi watakaosoma kozi hizo watapata fursa ya kusoma lugha mbalimbali za kigeni ikiwemo lugha ya Kireno,Kichina ,Kifaransa,Kijerumani,na kwamba chuo hicho pia kinatarajia kuanza kufundisha Programu ya lugha ya Kikorea.

 

 Hata hivyo amebainisha kuwa wakati wa udahili wa dirisha la pili wanatarajia kudahili wanafunzi kwa program mpya za Shahada ya Uzamili ya Benki na Fedha( MSc Benking & Finance) pamoja na Shahada ya Uzamili ya  Utawala wa Fedha na Biashara ( MBA-Finance).

 

" Ningependa kuwaomba wazazi wawalete wanafunzi  kwenye banda letu hapa Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wajionee kozi tunazofundisha ili wafanye maamuzi sahihi ya kujiunga na chuo chetu chenye fursa ya kupata ajira nje na ndani ya nchi" amesema Khadija.

 

Amewaondoa hofu wanafunzi watakaojiunga na chuo hicho kwani mazingira rafiki ya kujisomea katika kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo

 

No comments:

Post a Comment

Pages