August 20, 2022

Askofu amshauri Rais Samia, IGP



 Na Mwandishi Wetu

 

RAIS Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)   Camilius  Wambura  wameshauriwa kuwapandisha vyeo na mishahara askari  polisi wanaofanya  kazi kwa bidii na uadilifu kama njia muhimu ya kulijenga jeshi imara na la kisasa.  

 

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe  ya Maadili Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini  nchini Askofu William Mwamalanga wakati akizungumza na viongozi wenzake wa dini jana, mkoani Mbeya.

 

Amesema viongozi hao wanapaswa kutumia taarifa za utendaji wa askari ambao wanaonesha kuwa na weledi, bidii, uadilifu na nidhamu wakapandishwa vyeo na mishahara ili kuwa fundisho kwa wengine.

 

Mwenyekiti huyo amesema katika nchi zilizoendelea zinatumia kigezo cha kuwapa mishahara mizuri wafanyakazi wanaofanya vizuri, hivyo Tanzania inapaswa kufuata misingi hiyo.

 

Amesema maadili na uadilifu  kwa askari polisi ni muhimu ili kuhakikisha jeshi hilo linaendeshwa kwa weledi. 

 

Askofu huyo amesema wanashauri Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi (CCP), kiwe ni mahali pa kuimarisha maadili na uadilifu  kwa askari polisi wanafunzi  na wale ambao wanafeli somo hilo  arudishwe nyumbani.

 

Aidha Askofu Mwamalanga, amekemea vikali tabia ya baadhi ya  wananchi na wanasiasa   wanaochochea chuki dhidi ya polisi na kuwataka wasaidie jeshi hilo ili kuleta ufanisi.

 

Mwamalanga ameishauri jamii kutoa  taarifa za kweli ili kukomesha uhalifu  na kuvunja mitandao ya uhalifu wa pikipiki  maarufu bodaboda.

 

“Sisi viongozi wa dini  kote nchini tukitoa ushirikiano kwa jeshi la  polisia uadilifu na maad yataongezeka na askari watatokomeza uhalifu,” alisema.

 

Askofu Mwamalanga alitoa wito kwa viongozi wa dini kutojihusisha na uhalifu  ametoboa siri pale alipowataja baadhi ya viongozi wa dini kujihusha na vitendo vya uhalifu ndiyo maana watu kama hawa hawezi kwenda polisi kuwataja wahalifu.

 

“Tumekubaliana   kila dhehebu la dini kanisa na msikiti lazima  wawe na mtandao wa vijana unaopambana na uhalifu na ili kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale wabapobaini vitendo vya uhalifu,” alisema.

 

Alisema jeshi la Mkoa wa Mbeya linafanyakazi kubwa, ila changamoto iliyopo ni uchache wa vitendekazi, hivyo wanashauri Serikali kuyawezesha jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages