August 10, 2022

Benki ya NMB yaahidi kuendelea kutoa mikopo kwa wawekezaji sekta ya nishati nchini



 Afisa Mkuu wa Wateja wa Jumla Benki ya NMB, Alfred Shao akichangia mada ya “Umuhimu wa upatikanaji wa fedha na haki katika mamlaka” wakati wa Kongamano la Nishati lililofanyika jijini Dar es Salaam nakukutanisha wadau  wa sekta ya mafuta na gesi nchini.

 

Benki ya NMB imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kutoa mikopo kwa wadau katika mnyororo wa thamani wa sekta ya nishati nchini kwa lengo  la  kusaidia ukuaji wa sekta hiyo.

Akichangia mada ya “Umuhimu wa upatikanaji wa fedha na haki katika mamlaka” wakati wa Kongamano la Nishati lililofanyika jijini Dar es Salaam jana, Alfred Shao, Afisa Mkuu wa Wateja wa Jumla Benki ya NMB, alisema benki hiyo ina bidha nyingi za kifedha mahususi kusaidia wawekezaji watarajiwa katika sekta ya nishati chini.


Shao alisema benki hiyo ikiwa ni mshauri wa uwekezaji aliyeidhinishwa pia inatoa huduma za ushauri kwa wateja na pia wakati mwingine husaidia kutafuta mitaji kwa makampuni mapya.

“Sisi kama benki tunaelewa kuwa uwekezaji katika sekta ya nishati  unhitaji mitaji mikubwa. Tuna fedha za kutosha kutoa mikopo kwa wadau  kwenye sekta ya nishati.  Kwa sasa tunaweza kutoa mkopo wa mpaka bilioni 310 kwa mkopaji mmoja,” aliseme Shao.

Alisema benki hiyo pia imejenga ushirikiano mzuri na mashirika ya kifedha ya kimataifa kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) miongoni mwa wengine wanaopendelea hati fungani za kijani.

"Tulifanikiwa kutoa Hati Fungani Maaluum ‘NMB Jasiri Bond’ mwaka huu ambayo ilikuwa na mwitikio mzurim sana tunatarajia kutoa hati fungani ya kijani inayolenga sekta ya nishati jadidifu," alisema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Biashara na Uwekezaji Exaud Kigahe wakati wa hafla hiyo alisema Serikali inatarajia kutumia fursa kwenye maeneo ambayo hayajatumika hasa katika nishati jadidifu yaani renewable energy na kusisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kufanya kazi na sekta binafsi katika kukuza sekta hiyo.

Alisema Serikali tayari imeanza utekelezaji wa mkakati wa kuboresha mazingiraya kufanya biashara nchini Tanzania huku akisisitiza dhamira ya Serikali ya kupunguza urasimu usio wa lazima miongoni mwa taasisi zake.

“Kwa nchi yetu haipo kwenye kiwango kizuri cha mazingira ya kufanya biashara . Tumepiga hatua kubwa kuweka mazingira mazuri ya biashara kama sehemu ya juhudi zetu za kuvutia wawekezaji zaidi nchini na hii itatusaidia kuongeza ushindani," alisisitiza.



No comments:

Post a Comment

Pages