August 09, 2022

GF Trucks & Equipment LTD yazindua kampeni Kilimo Usafirishaji wakati wa Maonyesho ya Nanenane jijini Mbeya


Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s ltd, Smart Deus akiwakabidhi zawadi ya Tishet washindi wa shindano la Kilimo Usafirishaji lilifanyika katika viwanja vya Nane Nae jijini Mbeya wakati wa uzinduzi wa gari maalumu kwa wakulima lenye kauli mbiu  ya Kilimo  na Usafirishaji

Afisa Mauzo wa Kamapuni ya GF Trucks & Equipment’s ltd, Poul Msuku akigawa zawadi ya  Tishet  kwa mmoja ya mteja aliyefika bandani kwao wakati wa uzinduzi wa gari maalumu ya wakulima yenye lkauli mbiu ya KILIMO USAFIRISHAJI katika viwanja vya nane nane jijini Mbeya.
 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Wakati Maonyesho ya nane nane yakiendelea katika viwanja vya Jonh Mwakangale jijini Mbeya kampuni ya uuzaji wa magari na mitambo ya GF Trucks & Equipments Ltd imezindua kauli mbiu ya Kilimo Usarishaji katika viwanja hivyo yenye lengo la kuhamasisha wakulima kupata usafiri bora wa mazao yao.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi  huo Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo Smart Deus alisema kampuni hiyo imekuja na mkakati wa kuwakomboa wakulima wadogo na wajasiliamali kwa kuzindua gari mpya tani 4 aina ya  FAW  CA1073 maalumu kwa ajili ya kubebea mizigo midogo ambayo itawasaidia wakulima kutolea mizigo mashambani na  kuipeleka katika magulio na masoko

 

Pia  GF wanazo gari maalumu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji  hali ambayo itamwezesha mkulima kuendelea na shughuli za umwagiiliaji hata kama eneo husika  maji ya uhakika na hasa kipindi cha ukame Unajua kwa sasa Magari ya FAW yanatengenezwa nchini Tanzania katika kiwanda chetu kilichopo Kibaha mkoni Pwani hivyo kwa kununua magari  haya itawezesha serikali kuokoa pesa za kigeni zilizokua  zikitumika kuagiza magari kutoka nje ya nchi hali inayosababisha bei yetu kuwa rafiki tofauti na hapo awali alimaliza Smart Deus Meneja Masoko.

 

Kwa upande wa mmoja wa wakulima wa vitunguu katika bonde la Ruaha Iringa ,Samsoni Mwakibete  alisema ujio  na uzinduzi wa gari hiyo utawarahisishia wakulima katika shunghuli zao.

 

Gf wanampango maalumu wa kuwakopesha vitendea kazi wakulima kwa kushirikiana na Benki rafiki ambapo mkulima akikidhi vigezo atapatiwa mkopo wa huo na Benki itamlipia na dhamamana itakuwa kifaa hicho ambapo yeye na benki watamalizana wakati tayari anaendelea kufanyia kazi.

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages