August 18, 2022

Mbunge Koka aungana na UWT Kibaha kongamano la sensa


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na walishiriki wa kongamano maalumu la wanawake.

      Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliofika katika kongamano maalumu.

 

Na Victor Masangu, Kibaha

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, amewahasa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini kuhakikisha kwamba wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

 

Koka ameyasema hayo wakati wa kongamano maalumu lililoandaliwa na uongozi wa (UWT) Kibaha mji ambalo limehudhuliwa  na wanawake zaidi ya mia tano kutoka kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa serikali.

 

Mbunge huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo amesema wanawake pamoja na wananchi wote wanapaswa kujitokeza siku hiyo kwa lengo la serikali kuweza kupata idadi kamili ya watu wake ili iweze kuweza kupanga bajeti yake kwa usahihi.

 

"Kwanza kabisa napenda kuwashukuru wanawake wote wa UWT katika jimbo langu la Kibaha mjini kwa kuweza kujiitokeza kwa wingi katika kongamano hili kwa ajili ya sensa ya watu na makazi kwa hili Jambo ni muhimu Sana,"alisema Koka.

 

Pia Mbunge Koka alisema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba inatambua idadi ya watu wake wote ili iweze kuleta maendeleo katika nyanja mbali mbali hivyo ni muhimu wananchi wakajitokeza katika zoezi hilo.

 

Pia Koka amesema kuwa ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi wake wa Jimbo la Kibaha mjini katika kuhakikisha anawaletea chachu ya maendeleo katika miradi mbali mbali.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Elina Mngoja amesema kwamba lengo la kuandaa kongamano hilo ni kwa ajili kuweza kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa wanawake mbali mbali wa Kibaha.

 

Pia alisema kwamba katika kongamano hilo litaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwapatia wanawake hao waweze kupata fursa ya kujifunza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi.

 

Naye Mbunge wa viti maalumu Subira Mgalu aliwasihi wanawake wote wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi na kuongeza kwamba kufanya hivyo kutaisaidia serikali iweze kupanga mipango yake ya kimaendeleo.

 

Nao baadhi ya wanawake ambao wamehudhulia katika kongamano hilo wametoa pongezi kwa uongozi wa UWT pamoja na kumshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuweza kuweza kuwakutanisha kwa pamoja na kuwapatia elimu ya umuhimu wa sensa.

 

Kongamano hilo maalumu ambalo limeandaliwa na UWT Wilaya ya Kibaha limehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa chama Cha mapinduzi wakiwemo wabunge pamoja na madiwani.

 

No comments:

Post a Comment

Pages