August 19, 2022

Msanii MedMedko aja na kibao kuhamasisha Sensa

MSANII wa Muziki wa kizazi kipya Mediko Mbogela maarufu kama MedMedko anatamba na kibao cha kuwahamasisha watanzania kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan kwenda kuhesabiwa siku ya Sensa kitaifa Agosti 23, mwaka huu.

Pia, msanii huyo kupitia kibao chake hicho maarufu kama Sensa amewataka wakimbizi wa kisiasa walioko nje ya Tanzania akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kurejea nyumbani kwa ajili ya kuhesabiwa.

"Kama wote tulivyoona Rais Samia amefanya maridhino ya kisiasa Nchini,  wanasiasa akiwamo  Lissu wamekimbia kwa sababu za kisiasa hivyo hawana sababu za kubaki huko warudi nyumbani kuendelea na kuijenga nchi ikiwamo kushiliki zoezi la kuhesabiwa Sensa," alisema na kuongeza.

"Pia, nawaasa wale wanaoishi na watu wenye ulemavu wasiwafungie ndani bali wahakikishe wana pata haki ya  kuhesabiwa kama watanzania wengine  kwa sababu wote sisi ni walemavu watarajiwa" alisema Medmedko msanii kutoka jijini Mbeya.

Mbali na kibao cha Sensa kinachotamba katika vituo mbalimbali vya redio na mitandao ya kijamiii, msanii huyo ameshatoa vibao mbalimbali vinavyohusiana na matukio ya kitaifa pamoja na janga la Uviko 19 mwaka 2020 kijulikamacho kama Corona Virus ulifaya vizuri Nchini TZ na Kenya.


Kwa Sasa ametunga na kuimba wimbo wa Sensa  kwa madhumuni yaleyale ni kusaidia serikali katika kuelimsha jamii juu ya matukio au kampeni zinazo endeshwa kitaifa na kimataifa kwa lengo la Elimu na  Hamasa hiyo kuwafikia wanajamii wengi zaidi kama sehemu y kioo cha jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages