August 20, 2022

MWENGE WA UHURU KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KATA YA MASAKA IRINGA


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Saadan Kuwa Mwenge wa Uhuru Unaweza Kwenda Kuweka Jiwe la Msingi Katika ujenzi wa Bwawa Hilo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuhusu ujio wa  Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Saadan Kwenda Kuweka Jiwe la Msingi Katika ujenzi wa Bwawa Hilo.


Na Fredy Mgunda, Iringa

 

MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amesema kuwa mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan kata ya Masaka unaosimamiwa na uongozi wa Bonde la Rufiji.

 

Akizungumza wakati wa ziara ya waziri wa maji Juma Aweso alisema kuwa mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni mradi mkubwa na ambao unasimamiwa kwa ubora unatakiwa hivyo anaenda kuitarifu kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ili kufanikisha mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi.

 

Moyo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya maji imetoa fedha nyingi katika mradi huo hivyo unapaswa kupewa hadhi ya kitaifa kwa kuwa unaenda kutatua changamoto za wananchi wa kata ya Masaka na kata nyingine za jirani.

Akiwa katika ziara wilaya ya Iringa waziri waji Juma Aweso ameupongeza uongozi wa wilaya ya Iringa kwa kusimamia vizuri ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika bodi ya maji Bonde la Rufiji kwa kuwa litafanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi na kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa kata ya Masaka. 

Aweso alisema kuwa ameridhishwa na ujenzi wa mradi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan kwa kuwa mmoja ya miradi mingi mikubwa ambayo itakuja kuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi wanaolizunguka bwawa hilo. 

Aweso alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeiagiza wizara ya maji kuhakikisha inachimba mabwawa ya kila wilaya ili kutatua changamoto hiyo na kuongeza njia za kukuza uchumi wa maeneo husika. 

Alisema kuwa kukamilika kwa bwawa hilo kutaisaidia kuleta maendeleo ya miradi mingine ya maji kutokana na usimamizi mzuri ambao unafanywa na uongozi wa wilaya na mkoa kwa ujumla kwenye maendeleo ya miradi ya kijamii. 

Alisema mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua utagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni 900,982,000/= ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amezileta  kutatua changamoto hizo kwa wananchi wa kata ya Masaka. 

Aweso alisema kuwa wizara ya maji musimu huu wa kiangazi inajenga mabwawa kumi (10)ambapo mabwawa manne (4)yanajengwa katika wilaya ya chemba,mawili wilaya ya Bahi,wawili wilaya ya Chamwino na wilaya ya Iringa mabwawa mawili na wizara inafanya usanifu wa mabwawa 51 ambayo yanatarajiwa kujengwa katika mwaka ujao wa fedha 

Awali akisoma taarifa ya mradi kwa waziri,msimamizi wa mradi huo Eng Geofrey Simkonda alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni mkakati wa uendelezaji,utumiaji,uhifadhi na usimamizi wa vyanzo vya maji katika Bonde la Rufiji. 

Alisema kuwa lengo la ujenzi wa mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni kuvunia maji na kurahisiha upatikanaji wa maji kwa wananchi hususani wenye uhaba wa rasilimali za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kibinadamu. 

Eng Simkonda alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Iringa,kata ya Masaka inayojumuisha Vijiji vya Makota, Sadan na Kaning'ombe watanufaika na mradi huo. 

Alisema kuwa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua la Masaka lina kimo cha mita 14,urefu mita 260 na litakuwa na ujazo wa mita 439,803 na ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwaka 2022 hadi sasa mradi umefikia asilimia 50. 

 

No comments:

Post a Comment

Pages