August 07, 2022

RAIS AKOSHWA NA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA RC MBEYA

 

Rais Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la jenga la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Jenga la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililowekwa msingi na Rais Samia Suluhu Hassan.


NA IMMACULATE RUZIKA, MBEYA


Rais Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na ujenzi wa jengo la Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kusema kuwa ingawa wametumia Sh. Billioni 6 lakini jengo liko vizuri.

Rais Samia aliweka Jiwe la Msingi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya juzi Jijini hapa ambapo alisistiza ujenzi uendane na thamani ya jeo.

Rais Samia alisema alirushiwa picha ya jengo analoenda kuzindua alifurahishwa kwa kuona jengo limejengwa vizuri na kwa uhimara zaidi.
Aidha Rais Samia alisema kuwa wanaendelea kujengo majengo yaliyobora kwani hata majengo ya mahakama wameanza kuyaboresha.


‘’Jengo hili  limetumia Sh. Billioni 6,Mbeya ndio Makao Makuu ya Mikoa ya Nyanda za Juu lazima kuwe na je ngo zuri na tutaendelea kujenga majengo ya aina hii,katika  kila mikoa iliyokuwa Makao Makuu ya Kanda
‘’Nimeridhika na pesa ilivyotumika ,nawapa pongezi wanambeya, pesa ilivyotumika, imeendana na uhalisia’’, alisema Rais Samia
Mbeya niwaambie furaha yangu kuona jengo la Mkuu wa Mkoa, jengo hili litahudumia wananchi wengi.
Naye Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kandoro amesema kwanza anamshukuru Rais kwa kuzindua jengo hili, lakini wao ni wajibu wao kujenga majengo ya Serikali tena kwa ubora wa hali ya juu.
Arch. Kandoro alisema utayari wao upo wakati wote wanapohitajika kwani  ubunifu huu umeanzia ofisini TBA na  ubunifu wa mji wa Serikali Dodoma walifanya TBA na kushiriki kujenga.

No comments:

Post a Comment

Pages