Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (katikati),
akisikiliza maelezo ya namna mitambo ya kiwanda cha kuchakata mazao ya
nyuki inavyofanya kazi alipotembelea kiwanda hicho katika Wilaya ya
Bukombe Mkoani Geita leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin
Shigela pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali wakifuatilia.
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia)
wakifurahia jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary
Masanja (kushoto), wakati wa
mkutano na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita
kuhusu masuala ya uhifadhi na ufugaji nyuki.
Baadhi
ya wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb)
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu masuala ya uhifadhi
na ufugaji nyuki.
.
Na Mwandishi Wetu
Serikali
imejipanga kuja na mpango wa ufugaji nyuki ujulikanao kama Manzuki
ambapo nyuki watakuwa wanafugwa katika eneo maalum bila kuathiri
uhifadhi.
Hayo yamesemwa
leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)
alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe
Mkoani Geita.
Amefafanua kuwa kupitia mpango huo wananchi wataweza kufuga nyuki na kupata faida bila kuhama kuhama.
Kuhusu
wananchi wanaofuga nyuki katika Hifadhi ya Kigosi, amesema kuwa
Serikali imeruhusu wananchi kuendelea na shughuli za ufugaji nyuki
wakati inatafuta eneo mbadala la kuwahamishia wafugaji hao.
“Tamko
la Serikali ni kwamba shughuli za ufugaji nyuki zitaendelea hadi pale
tutakapotoa mbadala wa wapi mpeleke mizinga yenu.” Mhe. Masanja
amesisitiza.
Aidha,
amewataka wananchi kukitumia ipasavyo Kiwanda cha kuchakata asali
kilichopo katika eneo hilo ili waweze kuuza asali kwa faida.
Amewataka wananchi kutunza mazingira na kuacha kukata miti hovyo ili kuendelea kufaidika na mazao yatokanayo na nyuki.
Awali,
Waziri wa Madini na mbunge wa jimbo la Bukombe Mhe.Dkt.Doto Biteko
amesema, Mhe.Rais Samia anataka kuona kero za wananchi wakiwemo wa Uyovu
zinatatuliwa na ndiyo maana Mhe.Naibu Waziri amefika, hivyo kuwasihi
wananchi kuwa wahifadhi kwa kuilinda misitu ya Bukombe isiharibiwe.
Naibu
Waziri Mary Masanja anaendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa kwa
lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazoikabili Sekta ya
Maliasili na Utalii.
No comments:
Post a Comment