August 22, 2022

URA SACCOS YATOA VIFAA TIBA KWA JESHI LA POLISI TANZANIA


 Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Festo Mwinuki, akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba na kompyuta vilivyotolewa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi Tanzania (URA SACCOS), kwa ajili ya vikosi vya Jeshi la Polisi Tanzania, hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
 Kamanda wa Kikosi cha Bohari (ACP), Moses Mziray, akizungumza katika hafla hiyo.

Kamanda wa Kikosi cha Afya, (ACP), Hussein Yahya.

Kamanda wa Kikosi cha Afya, (ACP), Hussein Yahya, akionesha baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi Tanzania (URA SACCOS).
Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya URA SACCOS, Festo Mwikuni, akizungumza katika hafla hiyo.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Chama cha Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi Tanzania, URA SACCOS kimekabidhi vifaa tiba pamoja na kompyuta kwa vikosi vya Jeshi la Polisi Tanzania.


Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Jeshi hilo iliyopo Kunduchi, Simiyu na Kompyuta kwa ajili ya Kikosi cha Ufundi na kikosi cha Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi.

Akikabidhi katika hafla fupi iliyofanyika  katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya URA SACCOS, Festo Christopher Mwikuni amesema vifaa hivyo vinathamani ya Tsh. 40,361,000 ikiwa ni kutimiza takwa la kisheria la kurudisha faida kwa jamii inayowazunguka.

Amesema Bodi ya Chama hicho pamoja na wanachama wanaamini vitatumika kwa manufaa ya Jeshi la Polisi na wananchi kwa ujumla.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Afya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hussen Yahaya na Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Kamishna Msaidizi Fadhili Ishekazoba pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Bandari Kamishna Msaidizi Moses Mziray na Mkuu wa Kikosi cha Afya Kamishna Msaidizi Nyada Keshina kwa pamoja wamekishukuru Chama hicho kwa msaada huo kwani umekuja wakati muafaa.

No comments:

Post a Comment

Pages