September 02, 2022

BENKI YA CRDB YAZINDUA PROMESHENI YA TISHA NA TEMBO CARD JIJINI DODOMA

MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA wa Biashara Kanda ya Kati Jane Maganga,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro (Kusoto) akizindua  Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati.Kulia ni Meneja Mwandamizi Malipo ya Kadi kutoka CRDB Bw.Victor Makere hafla iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
 
MENEJA Mwandamizi Kitengo cha Kadi kutoka CRDB Bw.Karington Chahe,akielezea jinsi promosheni hiyo itakavyokuwa inafanyika mara baada ya kuzinduliwa kwa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma. Dodoma.
MTEJA wa CRDB Husna Mchana,ambaye ni mhudumu kutoka Kampuni ya Afroil Investment Pump,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akicheza burudani na wafanyakazi wa CRDB mara baada ya kuzindua  Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
 
 
***************
 
BENKI ya CRDB imezindua  Promosheni maalum ya matumizi ya kadi iliyopewa jina la “Tisha na TemboCard” kwa Kanda ya Kati itakayoendeshwa kwa kipindi cha miezi 3 kuanzia ilivyozinduliwa rasmi Kitaifa jijini Dar-es-Salaam mnamo Agosti 18, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma Meneja  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,amesema lengo la Promosheni hiyo ni kuwahamasisha wateja na Watanzania kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya manunuzi na malipo ya huduma.

Bi.Mishwaro amesema kuwa  bado watanzania wengi hawana mwamko wa kutosha juu ya matumizi ya kadi.

“Promosheni hii ina lengo la kuwahamasisha wateja na watanzania kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya manunuzi na malipo ya huduma huku wakijishindia zawadi,”amesema .

Aidha amezitaja  zawadi hizo ni fedha taslimu kila mwezi kwa wateja watatu ambapo watajishindia Sh.Milioni moja kwa mshindi wa kwanza, wengine washindi wawili watapata Sh.500,000 .

“Na kubwa zaidi ni safari ya kwenda nchini Qatar iliyolipiwa kila kitu kwa wateja wanne wa TemboCard, washindi ni wale tu watakaokuwa na miamala mingi kupitia kadi zao za TemboCard,”alisema.

Bi.Misharo amesema  kadi hizo zinatumika kupitia ATMs, matawi, CRDB Wakala, Mashine za malipo za (POS) na kufanya manunuzi na malipo kwa njia ya mtandao ndani na nje ya nchi.

''Ni matumaini yangu kuwa kampeni hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga utamaduni wa watu kutumia kadi zao kufanya malipo na manunuzi.''amesema 

Hata hivyo amewasihi wateja wote wenye kadi za TemboCard kufurahia urahisi wa kufanya malipo popote pale walipo huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi.

 Amesema kuwa wateja ambao hawana akaunti katika Benki ya CRDB huu ndio wakati wa kufungua akaunti na kuanza kuweka fedha ili kurahisisha kufanya miamala kupitia TemboCard zao ambazo watapewa baada ya kufungua akaunti. 

Naye , Meneja Biashara Kanda ya Kati, Jane Maganga, amesema kuwa promosheni hiyo ni ubunifu wa CRDB katika kuwarahisishia wateja wake kupata huduma mbalimbali.

“Hii promosheni ya Tisha na TemboCard ni shindano ambalo litampa mabadiliko mteja, atakuwa akihitaji huduma au bidhaa anatumia kadi yake kuchanja tu na kulipia badala ya kutoa burungutu la fedha,”amesema Maganga

No comments:

Post a Comment

Pages