September 21, 2022

CRDB, Wanahabari wakutana kujadili fursa za mitandao ya jamii




Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza katika semina maalum kwa waandishi wa habari, iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” iliyolenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari  za biashara na uchumi ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jami. Semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam leo. Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya waandishi 200 kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Meneja Mwandanimizi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo, akiendesha mijadala katika semina maalum kwa waandishi wa habari, iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” iliyolenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jami. Semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam leo. Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya waandishi 200 kutoka vyomb o mbalimbali nchini. Wengine pichani ni kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Ltd, Bakari Machumu,  Mkuu wa Idara ya Huduma ya Radio TBC, Asha Mbaruku, na Mhadhiri Chuo Kikuu Dar es salaam, Dkt. Darius Mukiza.

 

 Na Mwandishi Wetu

 

UONGOZI wa Benki ya CRDB umekutana wadau wa habari leo Septemba 20,2022 jijini Dar es Salaa kujadili namna mitandao ya kijamii inavyoweza kusaidia ukuaji wa biashara uchumi.

Mkutano huo uliopewa jina la siku ya vyombo vya habari na benki ya CRDB uliwakutanisha waandishi wa habari, wahariri kutoka vyombo tofauti, wahadhiri na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mkurugnzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB, Tulli Esther Mwambapa, amesema lengo la siku hiyo ni kuboresha uhusiano wa benki hiyo na waandishi wa habari uluodumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

“Sisi CRDB Benki tunavithamini sana vyombo vya habari na kuonesha hivyo tunawasaidia waandishi wenye sifa kuongeza elimu tunawapeleka nje ya nchi.

“Tunawekeza kwenye jamii na tunavyompa nafasi tunamtaka akirudi aje afanye kwa ajili ya jamii kupitia taaluma yake,” amesema Mwambapa.

Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo amesema siku hii itakuwa endelevu huku akisisitiza kuwa sekta ya habari ni muhimu kwa ustawi wa jamii hasa katika uchumi.

Aidha wadau hao pia wamejadili jukumu la vyombo vya habari katika kukuza uchumi ambapo waandishi nguli wa habari waliwataka waandishi wanaochipikia kuongeza ubunifu na kujituma bila kusubiri kuajiriwa.

No comments:

Post a Comment

Pages