September 23, 2022

KIDUKU, ABDO KHALED WAPIMA UZITO LEO

 

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

MASAA machache yamesalia kutoka hivi sasa kabla leo Jumamosi mabondia Twaha Kiduku na Abdo Khaled raia wa Misri kupanda ulingoni kuwania mkanda wa UBO Intercontinental katika Mtwara Ubabe Ubabe linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda wa Sijaona mkoani hapa.


Kiduku na Khaled wa wamepima uzito jana na tayari kwa pambano hilo la uzani wa Super Middle ambalo litachezwa kwa raundi 10 huku wa kazi wa mkoani hapa wakitarajia kushuhudia  kutoka kw mabondia hao.


Licha ya kuwepo kwa mapambano ya utangulizi ila bondia Karim Mandonga  amekuwa gumzo kubwa kwa watu wa mjini hapa kutokana na  umaarufu wa bondia huyo kutoka Morogoro kufuatia mikwara anayowapiga mabondia wenzake licha  ya kupokea vichapo mara kwa mara.

Kiduku amewahakikishia Watanzania kuwa yupo tayari kuwapa burudani ya ushindi kwenye pambano hilo wakati mpinzani wake akisema  kuwa atamaliza raundi kumi za pambano hilo kwa kuamini atamchapa mpinzani wake.


Mbali ya Kiduku, bondia Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ aliyepewa ubalozi wa mkoa wa  hapa, ameendelea kuonyesha umaarufu wake kuliko wanasumbwi wengine waliombatana. Mandoga  atacheza na Salim Abeid pambano la raundi nne, Adam Lazaro atatwangana na Francis Miyeyusho, Emiliano Polino atacheza na Osama Arabi.


Selemani Galile atapambana na Shaban Ndaro pambano la raundi sita, uzito wa kati, Nasra Msami dhidi ya Halima Bandola ikiwa ndiyo pambano pekee la wanawake likiwa la raundi sita.


Alto Kyenga atapambana na Ibrahim Tamba raundi sita, Malik Deo atacheza dhidi ya Bosco Bakari pambano la raundi nne, Paschal Manyota atazichapa dhidi ya Joseph Mchapeni. 

 

Mapambano mengine ni Shafii Mohamed dhidi ya Ramadhan Sunya, Iddi Pazi atacheza na Sebaatian Temba, Ayoub Mwankina dhidi ya Shaban Rajabu, Yassin Mbegu dhidi ya Hassan Mgaya. Azizi Salumu dhidi ya Biemo Max.

No comments:

Post a Comment

Pages