Imeelezwa kuwa ongezeko la wateja zaidi ya elfu 60 katika
kipindi cha miaka tisa kwa benki ya maendeleo nchini kumeifanya benki hiyo
kufikisha mali za thamani ya shilingi bilioni 102 huku ikifikisha amana ya
shilingi bilioni 72 hali inayo ifanya benki huyo kuwa mbioni kuingia katika benki
za kitaifa
Akizungumza leo jijini Dare slaamu katika hafala ya kutimiza miaka 9 ya benki ya maendeleo mkurugenzi mtendaji wa benii ya maendeleo nchini ibrahim mungalaba amesema benki hiyo imeendelea kukua kimtaji na wateja huku katika kipindi cha miaka tisa imechangia shilingi bilioni 10 kama kodi kwa serikali huku ikitoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 200.
Ameongeza Mkurugenzi kuwa maendeleo bank katika kipindi cha nusu ya mwaka benki hiyo
imepata faida ya zaidi ya shilingi milioni 754 huku wakitarajia ongezeko la
mara mbili kufikia mwisho wa mwaka na hivyo kuifanya kutoa gawio kubwa kwa wana hisa .
Pia amewataka watanzania na wateja wa benki ya maendeleo waendelee kuitumia benki hiyo kwani wamejipanga kuboresha huduma zake na kutanua wigo ili kuhakikisha maendeleo benki inamfikia kila mmoja ndani ya Tanzania.
Kwa upande wake mwakilishi wa askofu wa Dayosisi ya
mashariki na pwani ambao ndio waanzilishi wa benki hiyo frank kimambo ameeleza
kuwa mipango ya baadae ni kutanua wigo wa huduma matawi ya benki hiyo ili kutoa nafasi
kwa watazania kuhudumiwa na benki hiyo popote walipo kutoka matawi machache yaliyopo sasa.
No comments:
Post a Comment