September 07, 2022

Mama koka adhamiria kuanzisha Saccos ya wanawake wa uwt kibaha


Baadhi ya viongozi wa UWT Wilaya ya Kibaha mji wakiwa katika picha ya pamoja.

 

Na Victor Masangu, Kibaha

 

Mlezi wa umoja wa wanawake wa Chama Cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) Selina Koka ameahidi kushirikiana bega kwa bega na wanawake wenzake kwa lengo la kuweza kuleta chachu ya maendeleo na kukuza uchumi.

 

Selina ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ameyasema hayo Leo wakati wa baraza la la UWT lililoandaliwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake hao kutoka kata mbali mbali.

 

Alisema kwamba nia na dhamira yake ni  kuhakikisha anaweka mipango madhubuti ikiwemo kuanzisha Saccos ambayo itaweza kuwasaidia wanawake wa Jimbo la Kibaha mjini kujikwamua  kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.


 

"Kitu kikubwa ninachotaka kuwaambia Mimi Sina upendeleo na mwanamke yoyote yule lakini ninachotaka kusema kikubwa wakinama wasiniangushe lengo ni kujipanga kuanzia ngazi za kata ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi,"alisema Mama Koka.

 

Pia aliongeza kuwa katika kuwawezesha kiuchumi atatembelea katika kata mbali mbali na kupeleka wakufunzi kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na Mambo mengine yanayohusiana na maendeleo.

 

Aidha aliwataka wanawake wa UWT kuwa na vitega uchumi na kwamba atakuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi zao na atajitahidi kwa hali na mali  kufufua miradi ambayo imekwama katika ngazi ya kata.

 

"Kitu kikubwa wanawake wa UWT mnapaswa kuwa na mipango ya maendeleo ikiwemo Jambo la kuwa na vitega uchumi na hili jambo kwa upande wangu nitasaidiana na wenzangu katika Jambo hili,"alisema Selina.

 

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Mariam Mugasha alimpomgeza kwa dhati mlezi wao kwa juhudi zake na ushirikiano ambao anautoa kwa wanawake hao.

 

No comments:

Post a Comment

Pages