Janeth
Mashauri na Frank Kinabo kutoka Taasisi ya Mo Dewji Foundation,
wakimkabidhi Dk. Gerald Mongella, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya
Tumaini la Maisha mfano wa hundi ya Shilingi milioni 100. Ikiwa ni
mwendelezo wa ushirikiano baina ya Taasisi ya Mo Dewji na Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kupitia Taasisi Tumaini la Maisha kusaidia matibabu
ya watoto wenye saratani Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
Taasisi
ya Mo Dewji Foundation iliyoanzishwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji,
imetoa msaada wa Sh. Milioni 100 kwa ajili kusaidia matibabu ya watoto
wanaosumbuliwa na Saratani.
Akikabidhi msaada huo jijini Dar
es Salaam kwa Taasisi ya Tumaini la Maisha iliyopo katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Mkurugenzi wa Mo Dewji Foundation, Rachel Carp
amesema msaada huo unalenga kuboresha afya na kurejesha tumaini kwa
wagonjwa.
Rachel alisema mbali na kutoa msaada huo wa kifedha
wametoa sabuni za kufulia, kuogea na khanga ambazo wanaamini ni miongoni
mwa mahitaji muhimu kwa wahusika.
"Taasisi
ya Mo Dewji inaangazia elimu, maendeleo ya jamii, afya na uwezeshaji wa
kijinsia. Tunaamini kuwa huduma bora za afya zinazopatikana ni haki kwa
binadamu, na tumejitolea kuboresha huduma za afya hapa Tanzania"
amesema
Amesema tangu mwaka 2013, wameshirikiana na Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kupitia Tumaini la Maisha, Kituo Kikubwa zaidi cha
Saratani ya Watoto Afrika Mashariki.
Rachel amesemq wanaendelea
kufanya kazi na Tumaini la Maisha kwa sababu programu zao ni muhimu kwa
maisha ya watu wa nchi za Afrika Mashariki.
"Programu zao hutoa
huduma za kiafya na zisizo za kiafya kwa watoto, kama vile ununuzi wa
dawa za Kemotherapy, usaidizi kwa programu ya shule, matengenezo ya
mpango wa usafiri kwa wagonjwa na walezi wao, usaidizi wa programu ya
tiba ya michezo kwa wagonjwa, usaidizi katika mafunzo ya stadi za maisha
kwa wazazi, vifurushi kwa wagonjwa wapya waliolazwa, na usaidizi wa
mshahara kwa wafanyikazi ambao sio wa afya" amesema
Ametoa wito
kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi muhimu za Tumaini la Maisha na
mashirika mengine yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na
kuwawezesha watu wengi wasiojiweza nchini Tanzania.
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada wa sabuni za kufulia, kuogea na khanga,
Eliza Sanga ambaye ni mzazi wa mtoto anayepata matibabu ya Saratani
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema msaada huo ni mkombozi
kwao na kuwaomba Watanzania wengine kuiga moyo wa kujitolea kama
walivyofanya Mo Dewji Foundation.
"Tuna mahitaji ya muhimu mengi na baadhi yetu hatuna uwezo hivyo tunaposaidiwa tunafarijika zaidi" amesema.
Akipokea mfano wa hundi ya Sh. Milioni 100, Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya Tumaini la Maisha, Gerald Mongella amesema Mo Dejwi Foundation wameonyesha mfano mzuri wa kusaidia jamii yenye uhitaji hivyo amewaomba Watanzania wengine wahasike kusaidia matibabu ya watoto wenye saratani.
"Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu kwa kiwango ambacho kila mmoja anakihitaji lakini kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali malengo husika hufikiwa na jamii yenye shida hupata faraja" amesema.
No comments:
Post a Comment