Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB ,Ruth Zaipuna (katikati)
akinyanyua kombe juu kushangilia pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu
wa benki hiyo walipoishinda timu ya Bunge Sports Club kwenye bonanza la
kivumbi na jasho liliofanyika Jijini mwisho wa wiki ,NMB iliandaa
bananza hili lilishirikisha michezo mbalimbali kati ya Wabunge na
Wafanyakazi wa NMB, mechi hiyo ilichezwa uwanja wa Kilimani na michezo
mingene ilifanyika viwanja vya Chinangali Park.
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akikabidhi kikombe kwa timu ya mpira wa miguu ya NMB baada ya kuifunga timu ya Bunge Sports Club 2- -0 wakati wa mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya Kilimani jijini Dodoma kwenye Bonanza la NMB Kivumbi na Jasho. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna.
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
KIKOSI
cha timu ya soka ya NMB, kimeibuka wababe wa Tamasha la NMB-Bunge
Bonanza 2022 ‘Kivumbi na Jasho,’ baada ya kuwachapa wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Bunge FC’ kwa mabao 2-0 katika fainali
ya bonanza hilo, Jumamosi jioni, kwenye Uwanja wa Kilimani, jijini
Dodoma.
NMB-Bunge Bonanza ni tamasha la siku moja la michezo
baina ya timu za Benki ya NMB na Bunge, lililoanza kwa matembezi
yaliyoongozwa na Spika Dk. Tulia Ackson na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki
ya NMB (iliyoandaa bonanza hilo), Ruth Zaipuna, kabla ya timu za kila
upande kuchuana katika michezo mbalimbali.
Baada ya Bunge SC
kufanya vema katika michezo ya Kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku, Mpira wa
Wavu, Netiboli na Kikapu kwenye viwanja vya Chinangali Park, NMB ilikuja
juu na kupindua meza ya matokeo hayo kwa kushinda fainali ya soka kwa
mabao ya Alex Joseph na Laurent Kilumanga.
Ukiondoa ushindi huo,
NMB-Bunge Bonanza limefanyika kwa mafanikio makubwa, huku kila upande
miongoni mwa timu shiriki, ukilitumia tamasha hilo kufanya mazoezi ya
ushiriki wa matukio tofauti ya kimichezo, yanayohusisha timu za NMB na
Bunge SC.
Wakati Bunge SC, ikilitumia bonanza hilo kunoa makucha
kuelekea Mashindano ya tisa ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EALA 2022), timu za NMB wamelitumia kupasha misuli moto, kujiandaa na
Mbio za Hisani za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo.’
Akizungumza
wakati wa bonanza hilo, Spika Dk. Tulia alisema ya kwamba, wanaamini
NMB-Bunge Bonanza 2022 yatakuwa na mchango chanya kwa timu zao, kuelekea
EALA 2022 na kwamba walipanga kulipa uzito mkubwa ili kuhakikisha
linanufaisha timu zao, kama ilivyokuwa mwaka jana.
“Mwaka jana
tulishiriki Mashindano ya Mabunge na tuliongoza kwa ujumla, mafanikio
hayo yalitokana na ubora na uimara wa timu zetu, ambao ulianzia katika
NMB-Bunge Bonanza, na tunaamini limetupa mazoezi ya kutosha mwaka huu,
kutuwezesha kufanya makubwa zaidi ya msimu uliopita,” alisema Spika
Tulia.
Kwa upande wake, Zaipuna alisema timu zake zimeshiriki
bonanza hilo kama sehemu ya uenyeji wao wa Mbio za NMB Marathon,
zitakazofanyika hivi karibuni, Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, likilenga kukusanya Sh. Mil. 600 za kusaidia matibabu
ya kinamama wenye Fistula.
“Siku chache zijazo tutakuwa wenyeji
wa NMB Marathon, ndio maana tunalitumia bonanza hili kufanya mazoezi,
huku tukiwaomba Mheshimiwa Spika na Wabunge wote, mjitokeze kujisajili
ili kushiriki mbio hizo, zenye lengo la kukusanya pesa za kutibia kinana
mama wenye fistula katika Hospitali ya CCBRT,” alisema.
Licha ya NMB kuibuka na ushindi huo katika soka, pia ilishinda mchezo wa kufukuza Kuku wanaume, huku timu za Bunge zikitawala Michezo Mingine yote.
Katika Kikapu wanaume, Bunge iliibuka na ushindi wa pointi 44-40, huku upande wa wanawake Bunge nao wakishinda bada ya NMB kutoingiza timu uwanjani.
Michezo Mingine ambayo Bunge iliishinda NMB ni Kuvuta Kamba (wanawake na wanaume), netiboli 29-4, wavu wanawake na kufukuza Kuku wanawake.
No comments:
Post a Comment