September 27, 2022

Twiga awania kiti cha ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Kibaha mji

 

Mgombea wa nafasi ya mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Maryam Sheiban (Twiga).

 

Na Mwandishi Wetu, Kibaha


Aliyekuwa mlimbwende namba moja katika  kinyang'anyiro cha kumsaka miss Arusha kwa mwaka 2007 Maryam Sheiban almaarufu (Twiga) amejitosa kuwania kugombea nafasi ya mjumbe wa halmashauri halmashauri kuu ya chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji.

Mgombea huyo ambaye kwa sasa amekuwa mstari wa mbele katika kujishighulisha na mambo mbali mbali ya kijamii katika maeneo ya Kibaha pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla lengo ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu mjini kibaha ameahidi kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa kushirikiana na wanachama wenzake wa CCM.

"Lengo langu kubwa endapo nikifanikiwa kutetea katika nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM katika Wilaya ya Kibaha mji nitaweka mikakati madhubuti kwa kushirikiana na wenzangu katika kukiimarisha chama katika kuanzia ngazi ya chini,"alisema Twiga.

Pia alisema kwamba licha ya kuweka mipango dhabiti ya kukiimarisha chama pia ataendelea kusimamia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ili kuleta mageuzi ya kimaendeleo kwa wananchi wa Kibaha mjini pamoja na Taifa kwa ujumla.

Mgombea huyo amesema ana imani endapo atafanikiwa kushinda katika uchaguzi huo ataendelea kufanya mambo ya kijamii kwa kuwasaidia wananchi kutokana na mwongozo wa ilani ya chama inavyosema.

Aidha katika hatua nyingine alipongeza uongozi mzima wa chama Cha mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Kibaha mji kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega na wanachama katika kufanikisha dhamira ya kukitetea chama na kuwaletea wananchi maendeleo.

Sambamba na hilo mgombea huyo alimpongeza kaa dhati Rais wa awamu wa Sita Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo imeweza kuwasaidia wananchi wa Taifa la Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages