Na John Marwa
BAADA ya kufanikiwa kutinga hatua ya awali ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL. Mabingwa wa Tanzania Yanga SC wameangukia mikononi mwa Al Hilal ya Sudan.
Yanga wametinga hatua hiyo kwa kishindo kwa kuwachabanga Zalan FC ya Sudan Kusini mabao 9-0 na Sasa wanakutana na Al Hilal inayonolewa na mkongomani Florent Ibenge ambaye amewahi kuzinoa AS Vita Club na RS Berkane.
Wakati Yanga wakitakata Al Hilal wao wamewaondosha St George ya Ethiopia kwa faida ya bao la ugenini baada ya jana kushinda bao 1-0 na mchezo wa mkondo wa kwanza walipoteza mabao 2-1 na jumla matokeo yanawabeba Al Hilal.
Jambo zuri la kuvutia Yanga wanakutana na Al Hilal ya Ibenge ambaye anaujua ubora wa nyota wao wengi ambao wamewahi kupita kwenye mikono yake.
Hapa ndipo ubora na ugumu wa mechi unapokuja ukiachilia mbali ubora wa vikosi vyote viwili kwa namna walivuowekeza.
Yawezekana kikawa kipimo bora kwa Yanga licha ya ubora wa mchezaji mmoja mmoja. Yanga watanzia nyumbani kati ya Oktoba 7-10 kabla ya kwenda nchini Sudan katika mkondo wa pili.
Mshindi wa jumla wa michezo yote miwili anatinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.
Michezo mingine ambayo itapigwa katika hatua hiyo ya awali ni kama ifuatavyo.
Plateau Utd vs Espérance, Monastir vs Al Ahly, ASN Nigelec vs Raja Vipers vs TP Mazembe, Volcan Club vs Sundowns, Al Merreikh vs Ahli Tripoli, Agosto vs Simba SC, RC Kadiogo vs AS Vita na Cape Town City vs Petro Atletico.
No comments:
Post a Comment